Elimu

JINSI ya Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 (NECTA Form Six Results)

JINSI ya Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita

Matokeo Ya Kidato Cha Sita Pdf Download 2025: Jinsi ya Kuyapata Kwa Urahisi

Matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2025 yanaashiria hatua ya mwisho ya safari ya elimu ya sekondari kwa wanafunzi wa Tanzania. Mitihani hii ya ACSEE (Advanced Certificate of Secondary Education Examination) ni njia ya kuwapima wanafunzi kabla ya kujiunga na vyuo vikuu au kuingia katika soko la ajira.

NECTA (Baraza la Mitihani Tanzania) ndilo lenye jukumu la kutangaza matokeo haya rasmi kupitia mfumo wake wa mtandaoni na kwa njia mbadala kama USSD ili kuwafikia wote hata wale wasio na intaneti.

Hatua za Kuangalia Matokeo Ya Kidato Cha Sita Pdf NECTA

Ili kuangalia matokeo ya Kidato cha Sita kupitia mtandao, fuata hatua hizi:

1. Tembelea Tovuti Rasmi ya NECTA

Fungua kivinjari kisha andika: www.necta.go.tz

2. Nenda Sehemu ya “Matokeo”

Baada ya kufika kwenye ukurasa wa nyumbani, tafuta menyu au kiungo kilichoandikwa “Matokeo” au “Results”.

3. Chagua Matokeo ya ACSEE

Katika orodha ya mitihani, bonyeza sehemu ya “Matokeo ya ACSEE” ambayo ni kwa ajili ya Kidato cha Sita.

4. Chagua Mwaka wa Mtihani

Chagua mwaka 2025 ili kufungua matokeo ya mwaka husika.

5. Tafuta Shule Yako

Orodha ya shule zote zilizofanya mtihani huo itaonyeshwa. Tafuta jina la shule yako na bonyeza.

6. Angalia Matokeo Yako

Baada ya kufungua ukurasa wa shule yako, angalia jina lako ili kujua matokeo yako binafsi.

Njia Mbadala: Kuangalia Matokeo Kwa USSD

Kwa wale wasio na simu janja au huduma ya intaneti, NECTA pia inaruhusu kuangalia matokeo kwa kutumia USSD kwa hatua hizi:

  • Piga 15200# kwenye simu yako
  • Fuata maelekezo yatakayojitokeza kwenye skrini
  • Huduma hii inapatikana kwa gharama ya Tsh 100 kwa kila SMS

Link ya Haraka Kupata Matokeo

Pia unaweza kutumia kiungo hiki ili kufikia ukurasa wa matokeo moja kwa moja kupitia Habari Wise:
👉 Bofya Hapa Kuangalia Matokeo

🔔 Unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!

🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!