Nafasi 15 za Kazi ya Udereva Arusha City Council – Juni 2025
Arusha City Council imetangaza nafasi 15 za ajira kwa nafasi ya Dereva Daraja la II, kwa waombaji waliokidhi vigezo vya kielimu na uzoefu. Nafasi hizi ni fursa nzuri kwa Watanzania wanaotafuta ajira ya udereva katika taasisi za serikali.
Majukumu ya Kazi
- Kukagua hali ya usalama wa gari kabla na baada ya safari
- Kuwasafirisha watumishi wa halmashauri kwenye safari za kikazi
- Kufanya matengenezo madogo ya gari inapobidi
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali kwa wakati
- Kutunza kumbukumbu za safari zote kwenye daftari maalum
- Kuhakikisha usafi wa gari muda wote
Sifa za Muombaji
- Awe na cheti cha kidato cha nne (Form IV)
- Awe na leseni ya daraja C au E, na uzoefu wa kuendesha kwa angalau mwaka mmoja bila ajali
- Awe amehitimu mafunzo ya msingi ya udereva kutoka VETA, NIT au taasisi nyingine inayotambuliwa na serikali
Maelezo Muhimu ya Maombi
- Mwajiri: Halmashauri ya Jiji la Arusha
- Idadi ya Nafasi: 15
- Muda wa Kutuma Maombi: Kuanzia 18 Juni hadi 25 Juni 2025
- Mshahara: Kiwango cha TGS B/1
- Tuma Maombi Kupitia: portal.ajira.go.tz
🔔 Unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!