Ajira

NAFASI 4 za Kazi Kongwa District Council

NAFASI 4 za Kazi Kongwa District Council

Nafasi Mpya za Kazi Kongwa 2025: Halmashauri Yatangaza Ajira 4 za Msaidizi wa Kumbukumbu

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ametangaza ajira mpya kufuatia kibali kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi. Nafasi zinazotangazwa ni nne (4) kwa cheo cha Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II, ambapo waombaji wenye sifa wanakaribishwa kutuma maombi kupitia mfumo rasmi wa ajira kabla ya tarehe 26 Juni 2025.

Nafasi Zinazopatikana

Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – Nafasi 4

Sifa za Mwombaji

Mwombaji anatakiwa awe na Cheti cha Kidato cha Nne au Sita pamoja na Stashahada ya NTA level 6 katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali. Pia, anapaswa kuwa na ujuzi wa kutumia kompyuta.

Majukumu Makuu ya Kazi

  • Kusajili barua zinazoingia na kutoka kwenye rejista rasmi
  • Kusambaza majalada kwa maafisa husika na kuyapokea yanaporudishwa
  • Kutafuta na kurejesha kumbukumbu kwenye kabati au sehemu husika
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya taasisi

Mshahara

Mshahara utatolewa kulingana na ngazi ya Serikali ya TGS C.

Masharti kwa Waombaji

  • Mwombaji awe Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 45
  • Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kutaja aina ya ulemavu katika mfumo
  • Kuambatisha wasifu (CV), namba za simu na majina ya wadhamini watatu wa kuaminika
  • Kuambatisha vyeti halisi vilivyothibitishwa na Mwanasheria – cheti cha kuzaliwa, kidato cha nne/sita, stashahada, vyeti vya taaluma na cha kompyuta
  • Vyeti vya matokeo ya awali kama “Statement of Results” havitakubaliwa
  • Waliomaliza masomo nje ya nchi wahakikishe vyeti vimeidhinishwa na NECTA, TCU au NACTE
  • Wastaafu hawaruhusiwi kuomba isipokuwa wenye kibali maalum
  • Watumishi wa umma waliopo kwenye nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba
  • Maombi yenye taarifa za kughushi yatapelekea hatua za kisheria

Namna ya Kutuma Maombi

Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa ajira unaopatikana kwenye:
👉 https://portal.ajira.go.tz

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 26 Juni 2025. Maombi yoyote nje ya mfumo hayatazingatiwa. Waombaji wanapaswa pia kuambatisha barua ya maombi iliyoandikwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kwa anuani:

Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
S.L.P 57
KONGWA

🔔 Unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!

🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!