Matokeo ya Mock Darasa la Saba 2025: Angalia Orodha Kamili ya Mikoa
Matokeo ya majaribio ya darasa la saba kwa mwaka 2025 yameanza kutolewa katika baadhi ya mikoa nchini Tanzania. Haya ni matokeo muhimu kwa wanafunzi wanaojiandaa na Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE), unaoratibiwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).
Ingawa NECTA haina jukumu la kuandaa mitihani ya Mock, mitihani hiyo huandaliwa na ofisi za elimu za mikoa au wilaya. Lengo kuu ni kuwasaidia wanafunzi, walimu na wazazi kufahamu kiwango cha maandalizi ya mitihani ya mwisho. Kupitia matokeo haya, shule zinaweza kubaini maeneo yenye changamoto na kuchukua hatua za haraka kabla ya mtihani halisi.
Mikoa Iliyotoa Matokeo ya Mock Darasa la Saba 2025
Hadi sasa, baadhi ya mikoa imeshatangaza matokeo rasmi ya mitihani ya majaribio. Unaweza kufuatilia matokeo ya kila mkoa kupitia viungo vifuatavyo:
- Arusha Region: Tazama Matokeo
- Mbeya Region: Tazama Matokeo
- Morogoro Region: Tazama Matokeo
- Rukwa Region: Tazama Matokeo
- Ruvuma Region: Tazama Matokeo
- Geita Region: (Bado haijatolewa linki)
- Katavi Region: Tazama Matokeo
- Njombe Region: Tazama Matokeo
- Simiyu Region: Tazama Matokeo
- Songwe Region: Tazama Matokeo
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Mock Darasa la Saba 2025 Mtandaoni
Kuangalia matokeo ya Mock 2025 ni rahisi kwa njia ya mtandao. Fuata hatua hizi:
- Tembelea tovuti rasmi ya halmashauri ya wilaya au mkoa wako.
- Nenda kwenye sehemu ya Matangazo au Matokeo.
- Bofya kiungo kilichoandikwa “Mock Examination Results 2025”.
- Tafuta jina la shule au namba ya mtahiniwa kujua matokeo.
Kumbuka kutumia tovuti halali na zilizoaminika ili kuepuka taarifa potofu.
🔔 Je? unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!