Nafasi 9 za Kazi Zimetangazwa Wilaya Ya Rombo – Tuma Maombi Kabla ya Julai 7, 2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo ametangaza nafasi tisa (9) za ajira mpya baada ya kupokea kibali rasmi kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi wa Umma, kilichoidhinishwa tarehe 29 Aprili 2025. Tangazo hili linawalenga watanzania wote wenye sifa stahiki kuwasilisha maombi kwa nafasi mbalimbali zilizopo ndani ya halmashauri hiyo.
Jinsi ya Kupata Maelezo na Kutuma Maombi
Ili kujua majukumu ya kila nafasi, sifa zinazotakiwa na utaratibu wa kuwasilisha maombi, waombaji wanashauriwa kupakua tangazo kamili kupitia kiungo rasmi kilichotolewa:
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA TANGAZO
Tarehe ya Mwisho ya Maombi
Maombi yote yawe yamewasilishwa kabla au kufikia tarehe 7 Julai 2025.
Maelekezo Muhimu ya Kutuma Maombi
Waombaji wote wanapaswa kuambatisha barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na nakala za vyeti vya elimu. Barua hiyo ielekezwe kwa anuani ifuatayo:
MKURUGENZI MTENDAJI,
328 Barabara ya Sabasaba,
S.L.P 52,
25782 Mkuu – Rombo.
Ikiwa uko tayari kuanza safari mpya ya ajira serikalini, hii ni fursa ya kipekee kwa wanaotafuta kazi ndani ya sekta ya umma.
🔔 Unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!