Tetesi za Usajili Simba Leo: Orodha Kamili ya Majina
Dirisha kubwa la usajili kwa ajili ya msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/2026 linakaribia kufunguliwa, na tayari klabu ya Simba SC imeanza mipango madhubuti ya kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao, hasa kuelekea mashindano ya kimataifa ya CAF.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani, Simba pamoja na Yanga SC wamekuwa wakichuana vikali katika kumsaka vipaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), taifa linalotajwa kuwa kitovu cha wachezaji wenye viwango vya juu Afrika.
Katika msimu wa 2025/2026, Simba na Yanga zitaiwakilisha Tanzania Bara kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Azam FC na Singida Black Stars zikielekezwa katika Kombe la Shirikisho la CAF.
Kwa Simba SC, tayari kuna majina kadhaa yaliyowekwa kwenye rada kwa ajili ya kusajiliwa. Wengi kati yao ni viungo wa kati wenye uwezo mkubwa wa kucheza kama Defensive Midfielder (DM) au Attacking Midfielder (AM), huku lengo likiwa ni kuongeza nguvu na uzoefu ndani ya kikosi.
Orodha ya Wachezaji Wanaotajwa Kujiunga na Simba SC 2025/2026:
- 01. Feitoto (AM) kutoka Azam FC
- 02. Lassine Kouma
- 03. Abdalah Kulandana (DM) kutoka Fountain Gate FC
- 04. Balla Conte (DM) kutoka SFAXEN
- 05. Owen Tembo (DM) kutoka Power Dynamos
- 06. Abdou Seyd (DM) kutoka Binzertin
- 07. Ousine Badamasi (AM) kutoka TP Mazembe
Mwelekeo huu wa usajili unaonesha dhamira ya Timu ni kuingia kwa nguvu katika msimu mpya, kwa kuzingatia ubora na uzoefu wa wachezaji wanaolengwa. Uwekezaji huu wa mapema ni muhimu ili kuhakikisha timu inakuwa imara kimataifa na kuwapa mashabiki mafanikio wanayoyatarajia.
Ukifuatilia soka la Afrika, wachezaji kutoka DRC wameendelea kuleta ushindani mkubwa kutokana na uwezo wao wa kimwili, kiufundi na kiakili uwanjani. Hii ndio sababu Simba na Yanga wameelekeza macho yao huko, wakitarajia kupata mashine halisi za uwanjani.
🔔 Unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!