Nafasi 8 za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa 2025
Nafasi 8 za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa: Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ametangaza nafasi mpya 8 za ajira baada ya kupokea kibali kutoka kwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Utumishi. Watanzania wote wenye sifa wanakaribishwa kuomba nafasi hizi kwa kuzingatia vigezo vilivyoainishwa hapa chini.
Nafasi za Kazi Zilizotangazwa
1. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II β Nafasi 5
Majukumu:
- Kuchapa barua na nyaraka mbalimbali, zikiwemo za siri
- Kupokea wageni na kuelekeza wapi watapokea huduma
- Kutunza kumbukumbu za matukio, ratiba, na miadi ya ofisi
- Kupanga na kuandaa vikao
- Kuandaa orodha ya vifaa vya ofisi
- Kusambaza majalada na taarifa muhimu kwa idara husika
Sifa za Mwombaji:
Awe na elimu ya kidato cha nne pamoja na stashahada (Diploma) au cheti cha NTA Level 6 katika Uhazili. Lazima awe amefaulu Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza (100 maneno kwa dakika), na awe na ujuzi wa matumizi ya programu za ofisi kama Word, Excel, PowerPoint, E-mail, na Publisher kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali.
Mshahara: Ngazi ya TGS C
2. Dereva Daraja la II β Nafasi 3
Majukumu:
- Kukagua magari kabla na baada ya safari
- Kuwapeleka watumishi katika safari za kikazi
- Kufanya matengenezo madogo ya magari
- Kusambaza nyaraka na kutunza logbook
- Kusafisha gari na kutekeleza majukumu mengine ya udereva
Sifa za Mwombaji:
Awe na elimu ya kidato cha nne pamoja na leseni ya daraja E au C aliyotumia kwa zaidi ya mwaka mmoja bila ajali. Lazima awe na vyeti vya mafunzo ya udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na serikali.
Mshahara: Ngazi ya TGS B1
Vigezo vya Jumla kwa Waombaji
- Awe raia wa Tanzania mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 45
- Ambatishe cheti cha kuzaliwa na wasilisha CV iliyo na namba za simu na majina ya wadhamini
- Ambatishe vyeti vya kitaaluma na vya kidato cha nne au sita kulingana na kazi unayoomba
- Leseni ya daraja E au C lazima iambatishwe na cheti cha mafunzo ya udereva
- Testmonials na Statement of Results hazitakubalika
- Weka picha ya βpassport sizeβ kwenye mfumo wa Ajira
- Waombaji waliomaliza masomo nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na TCU, NECTA, au NACTE
- Wastaafu hawaruhusiwi kuomba bila kibali rasmi
- Walioko kwenye nafasi za kuingilia katika Utumishi wa Umma hawapaswi kuomba
- Atakayetoa taarifa za uongo atachukuliwa hatua za kisheria
Tarehe ya Mwisho ya Kutuma Maombi
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 13 Julai 2025.
Tazama tangazo kamili la PDF hapa
π Je? unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
π Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!