Klabu ya Simba inaendelea kufanya mabadiliko katika kikosi chake kwa kuwaacha baadhi ya wachezaji, idadi inayofikia wanane hadi tisa. Zifuatazo ni baadhi ya taarifa za wachezaji walioondoka na hatima zao.
Simba Yawapunguza Nyota Kadhaa: Nani Kaondoka, Nani Anaelekea Wapi?
Wachezaji Walioachwa na Simba
Orodha ya wachezaji walioachwa mpaka sasa inajumuisha majina yafuatayo:
- Ayoub Lakred
- Aish Manula
- Kelvin Kijili
- Valentino Nouma
- Omar Omary
- Okejepha
- Hamis Kazi
- Fabrice Ngoma
- Abel Hussein (Bado mchakato unaendelea)
Wachezaji wa Simba waliopewa Thank You
Pia, inatarajiwa kuwa mmoja wa mabeki wa kati wa kigeni na mmoja kati ya washambuliaji wawili waliopo kikosini wataondoka.
Manula Ajiunga Tena na Azam FC
Mlinda lango Aish Manula amerudi nyumbani kwa kujiunga na timu yake ya zamani, Azam Football Club (Azam FC). Hii ni hatua inayomrejesha Manula klabu aliyoitumikia awali kabla ya kujiunga na Simba.
Edwin Balua Aelekea Cyprus kwa Mkopo
Kiungo wa Simba, Edwin Balua, amefikia makubaliano ya kupelekwa kwa mkopo wa mwaka mmoja katika klabu ya Enosis Union Athletic Paralimni FC ya Cyprus. Mkataba huu wa mkopo unampa Balua fursa ya kudumu klabuni hapo endapo ataonyesha kiwango kizuri na kuwavutia waajiri wake wapya.
Enosis Union Athletic Paralimni FC ni timu inayoshiriki Ligi Kuu nchini Cyprus na ina historia yake katika mashindano mbalimbali. Kwa sasa, klabu hiyo inafanya usajili wa nguvu kwa lengo la kufanya vizuri zaidi msimu huu.
π Tafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
πΒ TembeleaΒ Habari WiseΒ kwa habari mpya kila siku!