Wabunge Waliokatwa na Kamati Kuu ya CCM Kwa Uchaguzi wa Ubunge 2025
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya uteuzi wa wanachama wake watakaoingia katika hatua ya kura za maoni kuwania nafasi za ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Tarehe 29 Julai 2025, chama hicho kimetangaza orodha ya wagombea waliopitishwa kuwania ubunge katika majimbo mbalimbali nchini.
Zoezi la Kura za Maoni
Wagombea waliotangazwa ndio watakaoshiriki katika zoezi la kura za maoni litakalofanyika kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025. Hii itasaidia kupata mgombea mmoja kutoka CCM atakayepigiwa kura na wananchi katika uchaguzi huo mkuu.
Orodha ya Wabunge Waliokatwa na CCM
Hapa chini ni baadhi ya majina ya wabunge waliokatwa na Kamati Kuu ya CCM na hatimaye hawajapewa nafasi ya kuwania ubunge tena kupitia chama hicho:
- Mrisho Gambo – Arusha Mjini
- Josephat Gwajima – Kawe
- Stephen Byabato – Bukoba Mjini
- Ndaisaba Ruhoro – Ngara
- Mohamed Monni – Chemba
- Christopher Sendeka – Simanjiro
- Lugaha Mpina – Kisesa
- January Makamba – Bumbuli
- Godwin Kunambi – Mlimba
- Justin Nyamoga – Kilolo
- Shanif Mansoor – Kwimba
- Idi Kassim Idi – Msalala
- Pauline Gekul – Babati Mjini
- Zubery Kuchauka – Liwale
- Emmanuel Ole Shangai – Ngorongoro
- Angelina Mabula – Ilemela
- Idd Mpakate – Tunduru Kusini
- Hasani Kungu – Tunduru Kaskazini
- Vedastus Mathayo – Musoma Mjini
- George Mwenisongole – Mbozi
- Nicodemas Maganga – Mbogwe
- Twaha Mpembenwe – Kibiti
- Shabani Shekilindi – Lushoto
- Innocent Kalogeres – Morogoro Kusini
- Dlatey Maasay – Mbulu Vijijini
- Alfred Kimea – Korogwe Mjini
- Taufiq Turkey – Mpendae
Matarajio ya Uchaguzi 2025
Wabunge waliopitishwa watapambana kuonyesha umahiri katika kura za maoni ili kuwa wagombea rasmi wa CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025. CCM inaendelea kuimarisha mchakato wa uchaguzi wake kwa kuhakikisha wagombea wenye umahiri na sifa wanachaguliwa kuwakilisha chama kwenye bunge.
🔔 Kwa habari mpya Kila siku. Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya habari kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!