Kuitwa Kazini

Majina ya Walioitwa Kazini CAMARTEC Agosti 2025: Orodha Kamili

Majina ya Walioitwa Kazini CAMARTEC Agosti 2025: Orodha Kamili

Majina ya Walioitwa Kazini Kituo cha CAMARTEC Mwaka 2025

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ametangaza orodha ya waombaji kazi waliofaulu usaili na kuteuliwa kwenda kazini katika Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC). Usaili huo ulifanyika kati ya tarehe 25 Mei hadi 5 Juni 2025.

Orodha ya Waliofanikiwa Kupangiwa Vituo vya Kazi

Majina yaliyotajwa katika tangazo rasmi yanahusisha waombaji waliopita usaili pamoja na baadhi waliokuwa kwenye kanzidata kwa kada mbalimbali ambao sasa wamepangiwa vituo baada ya nafasi kupatikana. Hii ni nafasi ya kipekee kwa waliochaguliwa kuanza safari yao katika utumishi wa umma.

Kupata Barua za Kuitwa Kazini

Waombaji wote waliopangiwa vituo wanapaswa kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal sehemu ya “My Applications” ili kupakua barua rasmi ya kupangiwa kituo. Ni muhimu kuchapisha barua hizo na kuziwasilisha kwa waajiri husika wakiwa na vyeti halisi vya taaluma kuanzia kidato cha nne.

Taratibu Muhimu za Kuripoti

Walioitwa wanatakiwa kuripoti kwa mwajiri ndani ya muda uliowekwa kwenye barua zao, wakiwa na nyaraka zote muhimu kwa ajili ya uhakiki kabla ya kupewa barua rasmi ya ajira.

Kwa wale ambao majina yao hayapo kwenye tangazo, wanashauriwa kutokata tamaa na waendelee kuomba nafasi nyingine zitakapotangazwa na Sekretarieti ya Ajira.

Pakua Tangazo Rasmi la CAMARTEC

Orodha kamili ya walioitwa kazini tarehe 01 Agosti 2025 inapatikana kupitia kiungo rasmi cha Ajira:

🔔 Tafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya za ajira kila siku!