Nafasi Mpya za Kazi Serikalini Kupitia Sekretarieti ya Ajira – Agosti 2025
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, inayofanya kazi chini ya Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kutoa matangazo ya ajira mpya serikalini kwa uwazi, usawa na kwa kufuata ushindani wa haki. Sekretarieti hii ina jukumu la kuhakikisha kuwa mchakato mzima wa ajira unaendeshwa kwa uwajibikaji na kwa kuzingatia viwango vya kitaifa vya ajira.
Fursa Sawa kwa Watanzania Wote
Kwa kutumia tovuti yake rasmi, Sekretarieti ya Ajira hutangaza nafasi mpya za kazi, taarifa za usaili na matokeo kwa lengo la kuwapa Watanzania taarifa kwa wakati na kuwasaidia kujiandaa ipasavyo. Hili limeiwezesha kuwa kiungo imara kati ya waajiri wa umma na watafuta kazi nchini, huku ikichochea uwajibikaji katika sekta ya umma.
Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri Mbalimbali Tanzania – Agosti 2025
Kwa mwezi huu wa Agosti 2025, nafasi mbalimbali za ajira zimetangazwa katika halmashauri na taasisi zifuatazo. Bonyeza kiungo husika kuona maelezo ya nafasi, sifa zinazotakiwa, na jinsi ya kutuma maombi:
- Tangazo la Kazi Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji – 01/08/2025
- Tangazo la Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu – 01/08/2025
- Tangazo la Kazi Halmashauri ya Mji wa Babati – 01/08/2025
- Tangazo la Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua – 01/08/2025
- Tangazo la Kazi Chuo cha Maji – 01/08/2025
- Tangazo la Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Iringa – 01/08/2025
Jinsi ya Kuomba
Waombaji wote wanashauriwa kusoma tangazo husika kwa makini, kutimiza vigezo vilivyowekwa, na kufuata utaratibu wa kutuma maombi kama ulivyoelekezwa kwenye tangazo husika. Hakikisha unawasilisha maombi yako kwa wakati kabla ya tarehe ya mwisho.
🔔 Tafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya za ajira kila siku!