Tangazo Muhimu: Mabadiliko ya Eneo la Usaili MOI kwa Tarehe 6 Agosti 2025
Ofisi ya Rais Yatangaza Mabadiliko kwa Waombaji Kazi MOI
Katibu wa Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ametangaza rasmi mabadiliko ya eneo la kufanyia usaili kwa waombaji kazi waliopangwa kufanyiwa mahojiano katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) mnamo tarehe 6 Agosti 2025.
Waombaji Watakiwa Kuhakikisha Wanazingatia Taarifa Mpya
Taarifa hiyo inawahusu waombaji wote waliokwisha kuitwa kwenye usaili, ambapo wanapaswa kuhakikisha wanazingatia eneo jipya lililopangwa kwa ajili ya zoezi hilo muhimu.
Kwa taarifa rasmi ya mabadiliko, waombaji wanashauriwa kupakua tangazo kamili kupitia tovuti ya ajira ya serikali:
👉 Bofya hapa kusoma MABADILIKO YA ENEO LA USAILI MOI
Angalizo kwa Waombaji
Waombaji wanahimizwa kufika kwenye eneo sahihi lililotajwa katika tangazo ili kuepuka usumbufu wowote na kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika hatua ya usaili kama ilivyopangwa.
🔔 Tafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya za ajira kila siku!