Orodha ya Wabunge Walioshinda Kura za Maoni CCM
Matokeo haya yanatokana na kura za maoni ndani ya chama cha CCM (internal primaries) na si uteuzi rasmi wa chama. Wagombea waliopata kura nyingi watapitia mchakato wa uteuzi kupitia Kamati Kuu ya CCM kabla ya kukubaliwa rasmi kuwania uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Wabunge Walioshinda Kura za Maoni CCM Mifano Muhimu
- Geita Mjini: Chacha Wambura alipata kura 2,145 akimshinda Constantine Kanyasu aliyepata 2,097
- Busanda: Dk Jafar Seif aliibuka na kura 5,286
- Same Mashariki: Anne Kilango alishinda kwa kura 3,029 dhidi ya Miryam Mjema (1,763)
- Bukoba Vijijini: Dk Jasson Rweikiza alipata kura 6,465 akimshinda Faris Buruhan (4,619)
- Tabora Mjini: Shabani Mruthu aliibuka na kura 6,612 dhidi ya Hawa Mwaifunga (326)
- Pangani: Jumaa Aweso alipata asilimia 100 ya kura zote (3,806)
- Arusha Mjini: Paul Makonda alipata kura 9,056
- Muheza: Hamisi Mwinjuma (MwanaFA) alipata kura 9,030 sawa na asilimia 91 ya kura halali
- Bukombe: Dk Dotto Biteko alipata kura takriban 7,456 (mgombea pekee)
- Nyasa: John Nchimbi alipata kura 9,157 dhidi ya Stellah Manyanya (548)
- Makambako: Daniel Chongolo alipata kura 6,151
- Rombo: Prof. Adolf Mkenda alipata kura 5,125
Wabunge Wengine Waliopata Ushindi
- Jesca David Kishoa (Iramba)
- Njalu Silanga (Itilima)
- Mohamed Mchengerwa (Rufiji)
- Abdulaziz Abood (Morogoro Mjini)
- Joshua Nassari (Arumeru Mashariki)
- Mary Daniel (Serengeti)
- Asia Halamga (Hanangβ)
Taarifa Zaidi Kuhusu Uchaguzi wa CCM
Matokeo haya ni hatua ya awali ya uteuzi ndani ya chama. Kamati Kuu ya CCM itapitia wagombea hawa kabla ya kutangaza rasmi majina ya wagombea wa uchaguzi mkuu ujao.
π Kwa habari mpya Kila siku. Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya habari kila siku!
π Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!