Michezo

Mohamed Hussein Ajiunga Rasmi na Yanga SC

Mohamed Hussein Ajiunga Rasmi na Yanga SC

Mohamed Hussein Atangazwa Rasmi Kujiunga na Yanga SC

Klabu ya Young Africans SC (Yanga) imethibitisha kumsajili rasmi beki wa kushoto wa Taifa Stars, Mohamed Hussein “Zimbwe Jr.”, ambaye ametua Jangwani kama mchezaji huru akitokea Simba SC.

Atua Yanga Baada ya Miaka 11 Simba SC

Zimbwe Jr., mwenye umri wa miaka 28, alikuwa nahodha wa Simba SC na ametumikia klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 11. Usajili wake Yanga SC umetangazwa rasmi usiku huu baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili, ambao utamuweka ndani ya Wananchi hadi Juni 2027.

Mohamed Hussein
Mohamed Hussein

Mchezaji wa Nane Kusajiliwa na Yanga Msimu Huu

Mohamed Hussein anakuwa mchezaji wa nane kusajiliwa na Yanga kuelekea msimu mpya wa 2025/2026. Kabla yake, klabu hiyo tayari imeshamsajili:

  • Mohamed Doumbia – Kutoka Majestic FC
  • Celestine Ecua – Kutoka Zoman FC
  • Andy Boyeli – Kutoka Sekhukhune United (Afrika Kusini)
  • Lassine Kouma – Kutoka Stade Malien
  • Abdulnasir “Casemiro” Abdallah Mohamed – Kutoka Mlandege (Zanzibar)
  • Offen Chikola – Kutoka Tabora United FC
  • Moussa Balla Conte – Kutoka CS Sfaxien (Tunisia)

Usajili wa Zimbwe Jr. unaongeza uzoefu mkubwa kwenye kikosi cha Yanga, ambacho kinajiandaa kwa msimu mpya wa mashindano ya ndani na kimataifa.

🔔 Kwa habari mpya za Michezo. Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya michezo kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!