Nafasi ya Kazi BBC Swahili: Mwandishi wa Habari wa Video
Shirika la BBC kupitia idara yake ya BBC Swahili, linatangaza nafasi ya kazi ya Mwandishi wa Habari (Digital Video Producer) kwa waombaji waliopo Tanzania. Nafasi hii ni ya kudumu na kwa muda wote, ikihusisha kazi za kutengeneza maudhui ya video kwa majukwaa ya kidijitali kama YouTube Shorts, TikTok, Instagram Reels, na Facebook.
Mwandishi atakayepatikana atawajibika katika kupendekeza, kuandika, kurekodi, kuhariri na kuchapisha video fupi na za kati, kwa kuzingatia hadhira ya kidijitali na viwango vya uhariri vya BBC.
Mahali pa kazi: Dar es Salaam, Tanzania (kwa kuhudhuria ofisini)
Mwisho wa kutuma maombi: 17 Agosti 2025
Waombaji wote lazima wawe na haki ya kufanya kazi nchini Tanzania.
Jinsi ya kutuma maombi:
Tembelea tovuti ya BBC kupitia kiungo hiki:
🔔 Je, unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya za ajira kila siku!