Michezo

Frank Assink Asaini Yanga SC kwa Mkopo

Frank Assink Asaini Yanga SC kwa Mkopo

Frank Assink Asaini Yanga SC

Klabu ya Yanga SC imethibitisha kukamilisha usajili wa beki wa kati raia wa Ghana, Frank Assink, akitokea Singida Black Stars kwa mkataba wa mkopo.

Kuimarisha Safu ya Ulinzi

Assink tayari ameanza mazoezi na kikosi kipya cha Yanga SC na anatarajiwa kuongeza nguvu kwenye eneo la ulinzi akishirikiana na Dickson Job, Ibrahim Abdallah na Bakari Nondo Mwamnyeto. Usajili huu unalenga kuimarisha safu ya nyuma ya Wananchi kuelekea mashindano ya msimu mpya wa 2025/2026.

Frank Assink Asaini Yanga SC
Frank Assink Asaini Yanga SC

Usajili wa Wachezaji Wapya Yanga 2025/2026

Frank Assink anakuwa mchezaji wa tisa kusajiliwa na Yanga SC kuelekea msimu wa 2025/2026. Kabla yake, Wananchi walishakamilisha usajili wa:

  • Mohamed Hussein kutoka Simba SC
  • Mohamed Doumbia kutoka Majestic FC
  • Celestine Ecua kutoka Zoman FC
  • Andy Boyeli kutoka Sekhukhune United (Afrika Kusini)
  • Lassine Kouma kutoka Stade Malien
  • Abdulnasir Abdallah Mohamed “Casemiro” kutoka Mlandege ya Zanzibar
  • Offen Chikola kutoka Tabora United FC
  • Moussa Balla Conte raia wa Guinea kutoka CS Sfaxien (Tunisia)
Frank Assink Asaini Yanga SC
Frank Assink Asaini Yanga

Usajili wa Assink unazidi kuimarisha kikosi cha Yanga SC ambacho kimepania kufanya vizuri ndani na nje ya mipaka msimu huu.