Bei Mpya za Mafuta Tanzania September 2025
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo mpya za bidhaa za mafuta ya petroli zitakazotumika kuanzia Jumatano, 3 Septemba 2025 saa 6:01 usiku. Bei hizi zinahusu rejareja na jumla kwa mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, huku bei za mikoa mingine zikibainishwa kwenye jedwali maalumu. EWURA Yatangaza Bei Mpya za Mafuta September 2025
Mwelekeo wa Bei za Mafuta Duniani
Kwa mwezi Septemba 2025:
- Bei za petroli zimepungua kwa 0.2%
- Bei za dizeli zimepungua kwa 5.5%
- Bei za mafuta ya taa zimepungua kwa 3.5%
Mabadiliko haya yanatokana na kushuka kwa gharama za mafuta yaliyosafishwa (FOB) katika masoko ya kimataifa.
Gharama za Uagizaji na Fedha za Kigeni
- Gharama za kuagiza mafuta (Premiums) zimeongezeka kwa wastani wa 20.73% kwa petroli, 7.75% kwa dizeli na 2.62% kwa mafuta ya taa katika Bandari ya Dar es Salaam.
- Bandari ya Mtwara haijabadilika, huku Tanga gharama zikishuka kwa 12.66% kwa petroli na dizeli.
- Kiwango cha kubadilisha fedha za kigeni (exchange rate) kimepungua kwa wastani wa 3.96%.
EWURA: Bei Mpya za Mafuta kwa Mwezi September 2025




Maelekezo ya EWURA kwa Wafanyabiashara
- Wafanyabiashara wote wa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zilizotangazwa rasmi na EWURA.
- Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka bango la bei inayoonekana wazi kwa wateja.
- Vituo vyote vya mafuta vinapaswa kuchapisha bei, punguzo na vivutio vya kibiashara vinavyotolewa.
- Mauzo yote ya mafuta lazima yatoe stakabadhi za EFPP zenye jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta na bei kwa lita.
Huduma za Kuthibitisha Bei
Wateja wanaweza kupata bei kikomo za mafuta kwa kutumia simu ya mkononi kwa kupiga:
*152*00#
→ kisha kufuata maelekezo.
Huduma hii ni bure na inapatikana kwenye mitandao yote ya simu nchini.
Ushindani na Ufuatiliaji
Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta 2015, kifungu 166, bei za mafuta zitaendelea kupangwa na soko, huku EWURA ikihakikisha haziwezi kuzidi bei kikomo au kushuka chini ya kiwango cha chini (floor price). Kampuni za mafuta zinaruhusiwa kushindana kibiashara kwa kutoa punguzo au huduma bora zaidi, mradi bei zao zibaki ndani ya viwango vya EWURA.
EWURA imesisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mfanyabiashara yeyote atakayekiuka maagizo haya.