Elimu

Majina ya Waliochaguliwa UDSM 2025/2026

Majina Waliochaguliwa UDSM 2025/2026

Majina ya Waliochaguliwa UDSM 2025/2026

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimetangaza rasmi majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Wakati huo huo, chuo kimefungua maombi ya awamu ya pili kuanzia tarehe 2 hadi 21 Septemba 2025. Waombaji wanatakiwa kuingia kwenye akaunti zao kupitia admission.udsm.ac.tz ili kuangalia hali ya uteuzi wao.

Maelekezo kwa Walioteuliwa

  • Waliochaguliwa na UDSM pekee: Wanafunzi hao watathibitishwa moja kwa moja.
  • Waliochaguliwa zaidi ya chuo kimoja: Wanapaswa kuthibitisha chaguo lao kupitia akaunti ya udahili kwa kuomba CODE, kuingiza namba hiyo na kubofya THIBITISHA.
  • Barua za kujiunga: Zitapatikana kuanzia 20 Oktoba 2025 baada ya mchakato wa uthibitisho kukamilika.

Tarehe Muhimu za Uandikishaji

  • 02 Septemba 2025: Kuanza kwa uthibitisho wa ofa.
  • 21 Septemba 2025: Mwisho wa kuthibitisha nafasi.
  • 01 Novemba 2025: Wiki ya elekezi kwa wanafunzi wapya.
  • 10 Novemba 2025: Mwanzo rasmi wa mihadhara.

Deadline za Udahili kwa Mwaka 2025/2026

  • July Intake: 30 Juni 2025
  • October Intake: 30 Septemba 2025
  • March Intake: 28 Februari 2026

Hitimisho

UDSM imepongeza wanafunzi wote waliopata nafasi ya kujiunga na chuo hicho kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Kwa waliokosa nafasi, dirisha la awamu ya pili bado liko wazi hadi 21 Septemba 2025.