JINSI ya Kufanya Marekebisho ya Majina ya Cheti cha NECTA Online
Utangulizi
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) linafanya marekebisho ya majina ya watahiniwa pale ambapo yamekosewa kuandikwa kwenye vyeti vya PSLE, CSEE na ACSEE. Utaratibu huu ni muhimu kuhakikisha jina lililo kwenye cheti linaendana na jina lililotumika katika mtihani wa awali.
Masharti ya Marekebisho ya Majina
- Ombi la marekebisho lazima lifanywe ndani ya mwaka mmoja baada ya matokeo kutangazwa.
- Marekebisho ni ya kufanya jina lifanane na lililotumika kwenye mtihani wa sifa (awali).
- Hayawezi kuwa ya kuongeza au kuondoa jina jipya.
- Marekebisho madogo ya herufi yasiyoathiri matamshi yanaruhusiwa.
- Kumbuka, cheti kilichokosewa lazima kirejeshwe NECTA.
Hatua za Kufanya Ombi la Marekebisho Online
- Tembelea tovuti ya NECTA: www.necta.go.tz
- Nenda kwenye E-services na uchague Replacement Certificate.
- Bonyeza Generate Control Number ili kupata nambari ya malipo.
- Weka taarifa zako kwa usahihi na bonyeza Save.
- Lipa ada ya Tsh 35,000/= kwa cheti kimoja kupitia benki au mitandao ya simu ukitumia Control Number.
- Baada ya malipo, chagua Correction of Names na bofya Apply/New.
- Ingiza nambari ya simu na Control Number.
- Jaza fomu ya maombi mtandaoni na bonyeza Submit.
Baada ya Marekebisho
Baada ya mchakato kukamilika, cheti kipya au slip ya matokeo yenye marekebisho kitatumwa kwa mkuu wa shule au kwa mtahiniwa husika endapo sio mwanafunzi.
Mawasiliano ya NECTA
- Anwani: Eneo la Viwanda Mikocheni, Barabara ya Bagamoyo, S.L.P. 2624 au 32019, Dar es Salaam
- Simu: +255-22-2700493-6/9, +255-22-2772423
- Nukushi: +255-22-2775966
- Barua pepe: [email protected]
- Tovuti: www.necta.go.tz