Jinsi ya Kujaza Fomu ya NIDA
Kujaza fomu ya NIDA ni hatua muhimu kwa kila Mwombaji wa Kitambulisho cha Taifa. Hapa kuna mwongozo wa hatua kwa hatua ili kuhakikisha mchakato unakamilika kwa usahihi. Kujisajili https://eonline.nida.go.tz/Account/Register
Mambo Muhimu ya Kuzingatia
- Barua Pepe: Tumia anuani halali ya barua pepe ili kujisajili na kupokea kiungo cha kuthibitisha akaunti.
- Nyaraka za Utambulisho: Lete nyaraka zisizopungua mbili, mfano cheti cha kuzaliwa.
- Muundo wa Nyaraka: Fanya skani (scanning) na weka nyaraka katika PDF (usizidi ukurasa mmoja kwa kila kiambatisho) au JPG/PNG.
- Namba ya Simu: Hakikisha umeweka namba sahihi ya simu.
- Vyeti vya Kuzaliwa: Wale waliozaliwa kuanzia 1980 na kuendelea wambatanishe cheti cha kuzaliwa; waliozaliwa kabla ya 1980 wambatanishe cheti cha kuzaliwa au affidavit.
- Majina ya Wazazi: Fahamu majina ya Baba na Mama. Wenye NIN za wazazi wambatanishe viambatisho halisi.
- Makazi: Jua namba ya nyumba, mtaa na kata unayoishi. Watanzania walioko nje wanatakiwa uthibitisho wa ukaazi kutoka ubalozi.
- Vyeti vya Ziada: Pasi ya kusafiria, leseni ya udereva, TIN, kadi ya mpiga kura, vyeti vya shule au chuo vinavyopatikana.
Hatua za Kujaza Fomu
- Jaza fomu ya maombi ya Utambulisho wa Taifa Namba 1A kwa kalamu ya wino mweusi na herufi kubwa.
- Hakikisha una saini fomu kwenye kipengele namba 59/60 au alama ya dole gumba kama huna saini rasmi.
- Gonga muhuri fomu yako kwenye Serikali ya Mtaa unakoishi.
- Ambatisha nyaraka muhimu kama cheti cha kuzaliwa, barua ya utambulisho wa makazi, cheti cha kuzaliwa au kitambulisho cha mzazi mmoja.
- Ambatisha viambatisho vingine vinavyopatikana, kama vyeti vya elimu, leseni ya udereva, kadi ya mpiga kura, kadi ya afya n.k.

Uchukuaji wa Alama za Kibaiolojia
- Fika Ofisi ya NIDA na nyaraka halisi.
- Chukuliwa alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki.
- Mavazi yanayopendekezwa: epuka rangi nyeupe, kijivu, bluu mpauko, pinki au nguo za kung’aa, jezi, nembo, kofia au kupaka hina viganjani.
Uhakiki na Pingamizi
- NIDA inachunguza taarifa zote na kupokea pingamizi kutoka kwa wananchi kuhusiana na waombaji.
- Pingamizi linaweza kuwasilishwa kwa barua, barua pepe au ofisi za wilaya husika.
Ugawaji wa Vitambulisho
- Baada ya kuthibitisha taarifa na kuchukuliwa alama za kibaiolojia, mwombaji hupatiwa Kitambulisho cha Taifa katika ofisi ya NIDA ya wilaya husika.
- Tambua risiti maalumu kutoka NIDA wakati wa hatua ya alama za kibaiolojia.
Mawasiliano na Maelezo Zaidi
- Simu: 0752 000 058 | 0687 088 888 | 0777 740 006 | 0677 146 666
- Tovuti: www.nida.go.tz
- Barua Pepe: [email protected]
- Mitandao ya Kijamii: Facebook, Instagram, Twitter @Nidatanzania
Kujisajili Mtandaoni
Mwongozo huu unahakikisha kwamba mchakato wa kujaza fomu ya NIDA, uthibitisho na kupokea Kitambulisho cha Taifa unakamilika bila tatizo.