Michezo

Viingilio Yanga Day 2025 – Mwananchi Day

Viingilio Yanga Day 2025 – Mwananchi Day

Viingilio Mwananchi Day 2025 – Yanga Day

Klabu ya Yanga SC imetangaza viingilio vya tamasha kubwa la Mwananchi Day 2025, litakalopigwa Ijumaa tarehe 12 Septemba 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Katika tamasha hilo, mashabiki watashuhudia utambulisho wa wachezaji na benchi la ufundi wa msimu mpya 2025/26, kisha kufuatiwa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Bandari FC ya Kenya kuanzia saa 11:00 jioni.

Viingilio vya Mchezo

  • Mzunguko: Tsh 5,000
  • Orange: Tsh 10,000
  • VIP C: Tsh 15,000
  • VIP B: Tsh 30,000
  • VIP A: Tsh 50,000 (SOLD OUT)
  • Royal: Tsh 300,000
  • VVIP: Tsh 600,000
Viingilio Mwananchi Day 2025 – Yanga Day
Viingilio Mwananchi Day 2025 – Yanga Day

Vituo vya Tiketi

Mashabiki wanaweza kupata tiketi katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwemo Jangwani, Ubungo, Kigamboni, Mbagala, Temeke, Ilala, Sinza, Leaders, Dar Live, na Mikocheni, pamoja na maduka ya TTCL na wasambazaji walioteuliwa nchi nzima.

Namna ya Kununua Tiketi kwa Mitandao ya Simu

Mashabiki pia wanaweza kulipia tiketi kupitia huduma za malipo ya simu kwa kutumia M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money na Halopesa. Unachohitaji ni kutumia N-Card yako na kufuata hatua zilizoainishwa kwenye menyu za malipo mtandaoni.

Kwa mashabiki wa Yanga na wadau wa soka nchini, Mwananchi Day 2025 inatarajiwa kuwa tamasha kubwa lenye shamrashamra, burudani na mpira wa kiwango cha juu.