Michezo

Matokeo Yanga vs Simba Leo 16/09/2025 Ngao ya Jamii

Matokeo Yanga vs Simba Leo 16/09/2025 Ngao ya Jamii

Matokeo ya Yanga vs Simba Leo 16/09/2025 Ngao ya Jamii

Septemba 16, 2025, uwanja wa Benjamin Mkapa umefurika mashabiki kushuhudia fainali ya Ngao ya Jamii 2025, inayokutanisha mahasimu wakubwa wa soka la Tanzania, Yanga SC na Simba SC. Hii ni mechi ya kufungua rasmi msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2025/2026, ikitajwa kuwa na mvuto wa pekee kutokana na historia, ushindani na rekodi za timu hizi mbili kongwe.

Umuhimu wa Ngao ya Jamii 2025

Ngao ya Jamii ilianzishwa na TFF mwaka 2001, ikihusisha bingwa wa ligi na mshindi wa Kombe la FA. Miaka ya karibuni, mashindano yalihusisha timu nne, lakini msimu huu TFF imepunguza washiriki kutokana na ratiba ngumu ya CAF na majukumu ya Taifa Stars. Fainali ya mwaka huu inazikutanisha Yanga na Simba pekee.

Rekodi za Yanga na Simba Ngao ya Jamii

  • Simba SC: Wameshinda Ngao ya Jamii mara 10, ikiwemo ushindi wao wa kwanza mwaka 2002 dhidi ya Yanga (4-1), na ushindi wa karibuni 2023 kwa penalti 3-1.
  • Yanga SC: Wameshinda mara 8, ushindi wa kwanza mwaka 2001 dhidi ya Simba (2-1), na ushindi wa karibuni 2024 walipoifunga Azam 4-1.

Kwa mara 9, timu hizi zimekutana fainali ya Ngao ya Jamii ambapo Simba wameshinda mara 5 na Yanga mara 4. Hii inafanya fainali ya 2025 kuwa na ushindani mkubwa kwani Yanga wanalenga kusawazisha rekodi huku Simba wakitaka kupanua mafanikio yao.

Waamuzi wa Mchezo

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kikosi cha waamuzi:

  • Mwamuzi wa kati: Ahmed Arajiga
  • Waamuzi wasaidizi: Mohamed Mkono na Kassim Mpanga
  • Mwamuzi wa akiba: Ramadhani Kayoko
  • Mtathmini wa waamuzi: Soud Abdi

Kauli za Makocha na Manahodha

  • Romain Folz (Yanga): Amesema kikosi chake kipo tayari kimwili na kiakili kwa ushindi licha ya wachezaji wachache kuwa majeruhi.
  • Fadlu Davids (Simba): Amedai presha ipo upande wa Yanga kutokana na matokeo ya karibuni, na Simba wako tayari kurejesha heshima yao.
  • Dickson Job (Yanga): Ametaja mchezo huu kuwa muhimu kwa kuashiria mwanzo wa msimu mpya.
  • Shomari Kapombe (Simba): Amesisitiza wanajua ubora wa Yanga na wamejipanga kuhakikisha wanapata matokeo chanya.

Wachezaji Watakaokosekana

  • Yanga SC: Pacome Zouzoua (majeraha).
  • Simba SC: Allassane Kante, Mohamed Semfuko na Mohamed Bajaber (majeraha).

Ratiba ya Mechi

  • Tarehe: 16 Septemba 2025
  • Saa: 11:00 jioni (EAT)
  • Uwanja: Benjamin Mkapa Stadium, Dar es Salaam

Hitimisho

Hii ni mechi inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki kote nchini, ikiwa ni Kariakoo Derby yenye historia kubwa. Habari Web Blog itakuletea taarifa zote za moja kwa moja kuanzia dakika ya kwanza hadi ya 90 ya fainali ya Ngao ya Jamii 2025 kati ya Yanga SC na Simba SC.

LIVE: Yanga SC vs Simba SC 16/09/2025