Matokeo ya Simba vs Yanga Leo 16/09/2025 Fainali Ngao ya Jamii
Hatimaye siku ambayo mashabiki wa soka nchini Tanzania wamekuwa wakingoja imewadia. Septemba 16, 2025, dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam limefurika mashabiki kushuhudia fainali ya Ngao ya Jamii 2025 inayowakutanisha mahasimu wa jadi Simba SC na Yanga SC. Huu ndio mchezo wa kufungua rasmi msimu wa 2025/2026 wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, ukitajwa kuwa wa kipekee kutokana na historia, rekodi na ushindani wa timu hizi kubwa.
Umuhimu wa Ngao ya Jamii 2025
Ngao ya Jamii imekuwa sehemu ya ratiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001. Awali ikiwakutanisha bingwa wa ligi na mshindi wa Kombe la FA, mashindano haya yamepitia mabadiliko kadhaa. Msimu huu TFF imeamua kushirikisha timu mbili pekee ili kupunguza msongamano wa ratiba kutokana na mashindano ya CAF na majukumu ya Taifa Stars katika kufuzu Kombe la Dunia 2026.
Rekodi za Simba na Yanga
Kwa upande wa takwimu, Simba imetwaa Ngao ya Jamii mara 10, ikiwemo ushindi wao wa kwanza mwaka 2002 dhidi ya Yanga kwa mabao 4-1, na wa karibuni mwaka 2023 walipoishinda Yanga kwa penalti 3-1. Yanga kwa upande wake imeibuka na taji hilo mara 8, mara ya kwanza mwaka 2001 ilipoifunga Simba 2-1, na mara ya mwisho mwaka 2024 dhidi ya Azam kwa ushindi wa 4-1.
Simba na Yanga tayari wamekutana mara tisa kwenye fainali za Ngao ya Jamii, ambapo Simba imeshinda mara tano na Yanga mara nne. Hivyo basi, mechi ya mwaka huu ni muhimu kwa Simba kuimarisha rekodi, huku Yanga ikiwinda kusawazisha.
Matokeo ya Simba vs Yanga Leo
Simba SC vs Yanga SC
Waamuzi wa Mchezo
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limethibitisha kikosi cha waamuzi kitakachosimamia Derby hii ya kihistoria. Mwamuzi wa kati atakuwa Ahmed Arajiga, akisaidiwa na Mohamed Mkono na Kassim Mpanga, huku mwamuzi wa akiba akiwa Ramadhani Kayoko. Mtathmini wa waamuzi ni Soud Abdi.
Kauli za Makocha na Manahodha
Romain Folz, kocha wa Yanga, amesema kikosi chake kipo tayari kwa burudani na ushindi licha ya changamoto za majeraha. Fadlu Davids, kocha wa Simba, amesisitiza kuwa presha ipo upande wa Yanga na kwamba Simba imejipanga kurejesha heshima yao. Nahodha wa Yanga, Dickson Job, amesema mechi hii inaashiria mwanzo wa msimu mpya, huku nahodha wa Simba, Shomari Kapombe, akiahidi matokeo mazuri kwa mashabiki wao.
Wachezaji Watakaokosekana
Yanga inaweza kumkosa Pacome Zouzoua kutokana na jeraha alilopata dhidi ya JKT Tanzania. Simba itawakosa Allassane Kante, Mohamed Semfuko na Mohamed Bajaber walioumia kwenye maandalizi ya msimu nchini Misri.
Ratiba ya Mechi
Mchezo wa Ngao ya Jamii 2025 utapigwa Septemba 16, 2025 saa 11:00 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Habari Web Blog itakuletea matokeo ya moja kwa moja (LIVE) Simba SC vs Yanga SC kuanzia dakika ya kwanza hadi ya 90.
LIVE Simba SC vs Yanga SC 16 September 2025