Matokeo ya Yanga vs Mbeya City Leo
Mashabiki wa soka walishuhudia mtanange mkali leo Jumanne, Septemba 30, 2025, katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, ambapo Mbeya City iliwakaribisha mabingwa watetezi Yanga SC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League).
Mchezo huo uliopigwa majira ya saa 10:15 jioni uliibua msisimko mkubwa kwa mashabiki kutokana na historia na ushindani wa timu hizi mbili.
Matokeo ya Mwisho
- FULL TIME: Yanga SC 0–0 Mbeya City
- Uwanja: Sokoine Stadium, Mbeya
- Tarehe: 30 Septemba 2025
- Saa: 10:15 Jioni
Hitimisho
Sare hii inawaacha Yanga SC na Mbeya City wakigawana pointi moja moja, huku ikiongeza ushindani kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC Tanzania Bara msimu wa 2025/2026.