Makala

Bei Mpya za Mafuta Tanzania Agosti 2025, EWURA

Bei Mpya za Mafuta Tanzania Agosti 2025

Bei Mpya za Mafuta Tanzania Agosti 2025 Zatangazwa na EWURA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetoa taarifa rasmi kwa umma kuhusu bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli zitakazoanza kutumika nchini kuanzia Jumatano, tarehe 6 Agosti 2025, saa 6:01 usiku.

Mabadiliko ya Bei Kwa Mikoa Mikuu

Kwa mwezi Agosti 2025, EWURA imetangaza bei mpya za rejareja na jumla kwa mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara. Mabadiliko haya yamezingatia mwenendo wa soko la dunia, gharama za uagizaji pamoja na viwango vya kubadilisha fedha za kigeni.

Tazama Bei za Mafuta Agosti 2025 Tanzania

Mwelekeo wa Bei Kwenye Soko la Dunia

Mabadiliko ya bei ya mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia kwa mwezi Agosti 2025 ni kama ifuatavyo:

  • Petroli: Imepungua kwa asilimia 2.3%
  • Dizeli: Imeongezeka kwa asilimia 5.5%
  • Mafuta ya taa: Yameongezeka kwa asilimia 3.7%

Gharama za Uagizaji Bandarani

Katika Bandari ya Dar es Salaam:

  • Petroli: Gharama imepungua kwa 12.43%
  • Dizeli: Gharama imepungua kwa 3.11%
  • Mafuta ya taa: Gharama imeongezeka kwa 13.08%

Katika Bandari ya Tanga:

  • Hakuna mabadiliko ya gharama

Katika Bandari ya Mtwara:

  • Petroli: Gharama imeongezeka kwa 6.12%
  • Dizeli: Gharama imeongezeka kwa 60.82%

Mabadiliko Katika Kiwango cha Kubadilisha Fedha

Gharama za mafuta zinalipiwa kwa fedha za kigeni, hasa Dola za Marekani. Kwa mwezi Agosti 2025, kiwango cha wastani cha kubadilisha fedha (exchange rate) kimepungua kwa asilimia 2.

Maelekezo kwa Wafanyabiashara wa Mafuta

EWURA imeelekeza kuwa:

  • Wafanyabiashara wa rejareja na jumla wauze bidhaa kwa bei ndani ya viwango vilivyowekwa (price cap)
  • Vituo vya mafuta viweke mabango ya bei yanayoonekana wazi kwa wateja
  • Mauzo yote yatolewe kwa kutumia Electronic Fiscal Pump Printer (EFPP) na wanunuzi wapate stakabadhi rasmi

Jinsi ya Kupata Bei ya Eneo Lako

Unaweza kupata bei kikomo ya mafuta kwa eneo lako kwa kupiga:

📱 15200#*
Kisha ufuate maelekezo. Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu nchini.

EWURA imesisitiza kuwa itaendelea kuhamasisha ushindani wa kibiashara kwa kutoa taarifa za bei kikomo na kuhimiza ufuatiliaji wa bei kwa njia rasmi.

🔔 Kwa habari mpya Kila siku. Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya habari kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!