Elimu

Download TCU Guide Book 2025/2026 kwa Udahili wa Shahada

Download TCU Guide Book 2025/2026 kwa Udahili wa Shahada

Download TCU Guide Book 2025/2026 kwa Waombaji wa Shahada

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetoa rasmi Undergraduate Admission Guidebooks kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Mwongozo huu ni muhimu kwa wanaotaka kujiunga na shahada ya kwanza katika vyuo vikuu vilivyoidhinishwa nchini Tanzania.

Kuhusu TCU

TCU ni taasisi iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Vyuo Vikuu ya 2005 (Sura 346) inayosimamia na kusimamia ubora wa elimu ya juu nchini. Mojawapo ya majukumu yake ni kuhakikisha mfumo wa elimu ya juu unaendeshwa kwa viwango vinavyokubalika kitaifa.

Aina za Guide Books Zinazopatikana

TCU imetoa miongozo hii mikuu mitatu ambayo unaweza ku-download kupitia tovuti yao rasmi:

1. Bachelor’s Degree Admission Guidebook kwa Wenye Stakabadhi za Kidato cha Sita (Form Six)

Download Guide Book kwa Form Six 2025/2026 (PDF)
Mwongozo huu unalenga wahitimu wa kidato cha sita wanaotaka kuomba kujiunga na vyuo vikuu.

2. Bachelor’s Degree Admission Guidebook kwa Wenye Diploma au Sifa Sawa na Hizo

Download Guide Book kwa Diploma 2025/2026 (PDF)
Mwongozo huu ni kwa waombaji waliomaliza elimu ya diploma au sifa sawa.

3. Bachelor’s Degree Admissions Almanac kwa Mzunguko wa Udahili wa 2025/2026

Download Almanac ya Udahili 2025/2026 (PDF)
Almanac hii ina ratiba kamili ya mchakato wa udahili mwaka mzima.

Jinsi ya Kufanya Download ya Mwongozo wa TCU

  1. Tembelea tovuti rasmi ya TCU kupitia https://www.tcu.go.tz
  2. Nenda sehemu ya “Public Notices”
  3. Chagua mwongozo unaohusika kulingana na sifa zako
  4. Fanya download ya faili la PDF ili uanze kusoma na kuandaa maombi yako

TCU inashauri waombaji wote kusoma kwa makini miongozo hii ili kufahamu vigezo vya kujiunga na programu husika na kufuata ratiba ya udahili iliyopo kwenye almanac.

🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!
🔔 Kwa habari mpya Kila siku. Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya habari kila siku!