Harmonize Atoa Wimbo Mpya “Coming Home” Wenye Ujumbe Mzito wa Hisia
Dar es Salaam, Tanzania – Mwanamuziki nguli kutoka Tanzania na Mkurugenzi Mtendaji wa Konde Music Worldwide, Harmonize, ameachia rasmi wimbo wake mpya unaoitwa “Coming Home”. Wimbo huu ambao tayari umeanza kupata mapokezi makubwa barani Afrika, unatoa ujumbe mzito wa hisia kuhusu mapenzi, uaminifu, na shauku ya kurudi kwa mpendwa.
“Coming Home” unagusa nyoyo za wengi kutokana na ujumbe wake wa dhati. Harmonize ameonyesha ukomavu wake wa kimuziki kwa kuchanganya vema staili yake ya Bongo Flava na midundo ya Afrobeat, na kutengeneza wimbo mtulivu lakini wenye hisia kali. Mashairi ya wimbo yanaelezea safari ya kuondoka mbali na mpendwa, hisia za kumkumbuka, na hatimaye, kurudi mahali ambapo moyo unastahili kuwa. Ujumbe huu unaaminika kuwafikia mashabiki wengi ambao wamepitia au wanapitia hali kama hizo katika maisha yao ya mahusiano.
Harmonize ameendelea kudhibitisha nafasi yake kama mmoja wa wasanii wakubwa na wenye ushawishi mkubwa katika tasnia ya muziki Afrika. Wimbo huu mpya unatarajiwa kuendelea kuweka rekodi nzuri katika chati mbalimbali za muziki na kuongeza idadi ya vibao vyake vikali.
Unaweza kusikiliza wimbo “Harmonize – Coming Home” hapa chini;