JEZI Mpya za Simba SC Msimu wa 2025/2026, Uzi Mpya wa Simba SC 2025/2026
Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema kuwa uzinduzi wa jezi Simba za msimu 2025/2026 zitazinduliwa Agosti 27 katika ukumbi wa Super Dome Masaki kuanzia saa moja usiku.
Ahmed amesema safari hii itakuwa tofauti na kila ambaye atahitaji kushiriki tukio hilo atatakiwa kulipia Shilingi 250,000 ambapo kutakuwa na burudani za kutosha.
Ahmed ameongeza kuwa atakayelipa kiingilio hicho atapata jezi zote tatu za msimu yaani nyekundu, nyeupe, na bluu, chakula, vinjwaji pamoja na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali na Live Band.
Aidha Ahmed ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa zoezi la utambulisho wa jezi zetu litaongozwa na Mgeni rasmi ambaye ni nyota wa zamani wa soka aliyetikisa Afrika na Dunia na hilo linazidi kulifanya tukio hilo kuwa la Kimataifa.
Aidha Ahmed Ally amesema kuwa Kwa kuwa ukumbi wa Super Dome unahitaji kiwango cha watu maalum hivyo watakaohitaji kushiriki wapige namba 0794160000 au 0675666333 na idadi ikifikiwa zoezi litafungwa.
Baada ya zoezi hilo la uzinduzi kukamilika jezi zitauzwa katika maduka yote nchi nzima ambayo yalikuwa wameweka oda na bei ya rejareja itakuwa Shilingi 45,000.