Jinsi ya Kurejesha Mkopo Kupitia Mfumo wa OLAMS
Mfumo wa OLAMS wa HESLB umeundwa kurahisisha ulipaji wa mikopo ya elimu ya juu. Kupitia mfumo huu, wanufaika wanaweza kujisajili, kuthibitisha taarifa zao na kufanya malipo kwa njia salama na rahisi.
👉 Ingia moja kwa moja kupitia kiunganishi: olas.heslb.go.tz
Hatua za Kufanya Usajili
- Chagua Loan Beneficiaries
- Tengeneza akaunti mpya
- Chagua aina ya usajili – mfano: Loan Repayment
- Jaza namba sahihi ya mtihani wa Kidato cha Nne (Form Four Index Number)
- Jaza barua pepe yako na namba ya simu
- Tengeneza nywila (password) na bofya Register
- Kisha ingia tena kwa kubofya Log in as Registered User
Hatua za Kufanya Malipo
- Ingia kwa kutumia namba ya mtihani wa kidato cha nne na nywila yako
- Chagua LIPA
- Jaza taarifa zako za ajira:
- Aina ya ajira: Umma / Binafsi / Umejiajiri
- Mkoa
- Check Namba (kwa watumishi wa umma)
- Mwajiri wako
- Namba ya simu na barua pepe
- Hifadhi taarifa zako kisha endelea na malipo
Jinsi ya Kupata Taarifa ya Deni (Customer Statement)
- Bofya Customer Statement
- Taarifa ya deni lako itaonekana mara moja
Jinsi ya Kulipa Deni
- Bofya Make Repayment
- Jaza kiasi cha fedha unachotaka kulipa
- Jaza namba ya simu na barua pepe
- Tumia namba ya kumbukumbu ya malipo uliyopewa kufanya malipo kupitia benki au simu ya mkononi
Mawasiliano ya HESLB
Kwa msaada zaidi, wasiliana na HESLB kupitia:
- Simu: 0736 66 55 33
- WhatsApp: 0739 66 55 33
- Barua pepe: [email protected]
Kwa kutumia mfumo wa OLAMS, ulipaji wa mkopo wa HESLB umekuwa wa haraka, salama na rahisi kufuatilia popote ulipo.