Kwa urahisi zaidi, Klabu ya Yanga SC imewezesha mashabiki wake kununua tiketi za Yanga Day 2025 kupitia huduma za mitandao ya simu bila kulazimika kufika vituoni.
Hatua za Kununua Tiketi za Yanga Day 2025
Mashabiki wanaweza kutumia huduma zifuatazo:
1. M-Pesa
- Piga 15000#
- Chagua Lipa kwa M-Pesa > Zaidi > E-payment
- Chagua Tiketi za Mpira
- Chagua mechi unayotaka kulipia
- Ingiza namba ya kadi yako ya N-Card
- Weka namba ya siri na thibitisha
2. Tigo Pesa
- Piga 15001#
- Chagua Lipa Bill > Malipo Mtandaoni
- Chagua Tiketi za Mpira
- Chagua mechi na aina ya tiketi
- Ingiza namba ya N-Card na thibitisha
3. Airtel Money
- Piga 15060#
- Chagua Lipa Bill > Malipo Mtandao
- Chagua Football Tickets
- Chagua mechi na aina ya tiketi
- Weka namba ya N-Card na thibitisha
4. Halopesa
- Piga 15071#
- Chagua Lipa Bill > Malipo Mtandaoni
- Chagua Tiketi za Mpira
- Chagua mechi, aina ya tiketi
- Ingiza namba ya N-Card na thibitisha
Kwa njia hii, mashabiki wanaweza kupata tiketi kwa urahisi na usalama, popote walipo nchini.