Jinsi ya Kuomba AVN, NACTVET Award Verification Number
Namba ya Utambulisho wa Tuzo (AVN) ni muhimu kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kupitia Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET). Wengi husubiri hadi kipindi cha udahili, lakini unaweza kuomba AVN mara tu baada ya matokeo yako ya diploma kufanyiwa uhakiki.
Hatua za Kuomba AVN
- Tembelea tovuti ya NACTVET kupitia www.nactvet.go.tz
- Bofya Request Award Verification Number kwenye sehemu ya key links
- Jaza taarifa zako kwa usahihi kulingana na maelekezo yaliyopo
- Fanya malipo kwa kutumia namba ya malipo utakayopatiwa
- Hifadhi namba ya tuzo (AVN) utakayotumiwa kwa ajili ya udahili kwenye chuo unachokusudia kujiunga nacho

Hitimisho
Ni vyema kuomba AVN mapema badala ya kusubiri hadi kipindi cha udahili. Hii itakuokoa muda na changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa mchakato wa kujiunga na vyuo.