Makala

Jinsi ya Kupata Kitambulisho cha NIDA Kilichopotea

Jinsi ya Kupata Kitambulisho cha NIDA Kilichopotea

Jinsi ya Kupata Kitambulisho cha NIDA Kilichopotea

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imetoa mwongozo kwa wananchi kuhusu hatua za kufuata pale kitambulisho cha taifa kinapopotea, ili mtu aweze kupata kitambulisho kipya. Hatua hizi ni muhimu hasa kwa wale wanaohitaji vitambulisho vyao kufanikisha huduma nyingine kama pasipo za kusafiria za kielektroniki.

Hatua Muhimu za Kufuata

  1. Taarifa Polisi: Kila mtu aliyepoteza kitambulisho chake anatakiwa kwanza kutoa taarifa kwa polisi. Hii itakuwa Loss Report ya upotevu wa kitambulisho.
  2. Malipo: Gharama ya kupata kitambulisho kipya ni TZS 20,000/=, inayolipwa baada ya kupata fomu kutoka ofisi ya NIDA.
  3. Kusajili na Kuomba Kitambulisho Kipya: Baada ya kupata Loss Report na kufanya malipo, mlaji anapaswa kuwasilisha hati hizo kwenye ofisi ya usajili ya NIDA ili kuanza mchakato wa kutengenezewa kitambulisho kipya.
Kupata Kitambulisho cha NIDA Kilichopotea
Kupata Kitambulisho cha NIDA Kilichopotea

Maelezo Zaidi

  • Fika kwenye ofisi ya usajili ya wilaya yako au ile ulijisajili, utapewa fomu ya polisi na fomu ya malipo ya akaunti.
  • Baada ya kukamilisha malipo, wasilisha Loss Report na hati ya malipo kwa ofisi ya NIDA kuanza utengenezaji wa kitambulisho kipya.

Kupoteza kitambulisho cha NIDA hakipaswi kusababisha hofu, lakini ni muhimu kufuata hatua hizi rasmi ili kupata kitambulisho kipya haraka na salama.