
Kikosi cha Simba Dhidi ya Yanga Leo 16/09/2025 Fainali Ngao ya Jamii
Hatimaye, siku kubwa kwa mashabiki wa soka nchini imefika. Fainali ya Ngao ya Jamii 2025 inakutanisha mahasimu wakuu wa soka la Tanzania, Simba SC na Yanga SC, leo Jumanne 16 Septemba 2025, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Mashabiki wa pande zote mbili wanatarajiwa kujaza uwanja huo huku kila mmoja akisubiri kuona kikosi chake kikianzia msimu mpya wa 2025/2026 kwa kishindo.

Kikosi cha Simba Vs Yanga Leo Ngao ya Jamii
Kikosi cha Simba Leo
- 26 CAMARA
- 12 KAPOMBE C
- 30 NABY
- 14 HAMZA
- 23 DE REUCK
- 21 KAGOMA
- 38mKIBU
- 8 KANTE
- 11 MUKWALA
- 10 AHOUA
- 34 MPANZU
SUBS:
YAKOUB, CHASAMBI, MLIGO, CHAMOU, NANGU, MZAMIRU, MAEMA, MWALIMU, MORICE, MUTALE.
Kikosi rasmi cha Simba kitakachoshuka dimbani kinatarajiwa kuthibitishwa saa 10:00 jioni, huku nyota kama Jean Charles Ahoua, Steven Mukwala na Ellie Mpanzu wakitarajiwa kuanza mechi hii muhimu.
Umuhimu wa Mchezo
Ngao ya Jamii mwaka huu ni ya kipekee kwa kuwa tofauti na toleo la 2024 lililohusisha timu nne, safari hii imebaki fainali moja pekee. Hali hii inaongeza hamasa na presha kwa wachezaji na makocha kwani mchezo huu ni mwanzo rasmi wa mashindano yote yanayosimamiwa na TFF msimu huu.
Historia ya Ngao ya Jamii
Ngao ya Jamii ilianzishwa mwaka 2001 kwa pambano la kwanza kati ya Simba na Yanga, ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1. Tangu hapo, mashindano haya yameendelea kuwa kipimo cha mwanzo wa msimu mpya. Katika kipindi cha miaka 20, Simba na Yanga wamekutana mara tisa kwenye fainali, Simba ikishinda mara tano na Yanga mara nne.
Rekodi za Simba na Yanga
- Simba SC: Imetwaa Ngao ya Jamii mara 10, ikiwa na ushindi wa kwanza mwaka 2002 dhidi ya Yanga kwa mabao 4-1. Ushindi wao wa hivi karibuni ulikuwa 2023 kwa penalti 3-1 baada ya sare tasa.
- Yanga SC: Imetwaa Ngao ya Jamii mara 8, ikiwemo ushindi wa mwaka 2024 ilipoifunga Azam mabao 4-1.
Hitimisho
Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa wa kukata na shoka. Simba inalenga kuongeza rekodi yake, huku Yanga ikisaka usawa wa historia. Bila shaka, Ngao ya Jamii 2025 itakuwa pambano lenye ushindani mkubwa linaloashiria mwanzo wa msimu mpya wa soka Tanzania.