Michezo

Kikosi cha Taifa Stars CHAN 2024: Wachezaji Kuungana Kambini Julai 7, 2025 Misri

Kikosi cha Taifa Stars CHAN 2024
Kikosi cha Taifa Stars CHAN 2024: Wachezaji Kuungana Kambini Julai 7, 2025 Misri

Kikosi cha Tanzania kitakachoingia kambini Julai 7, 2025, Misri kwaajili ya michuano ya CHAN 2024

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kikosi cha wachezaji kitakachoingia kambini kuanzia Julai 7, 2025 nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya CHAN 2024. Mashindano hayo yatafanyika kwa pamoja katika mataifa matatu ya Afrika Mashariki—Kenya, Tanzania, na Uganda.

Kocha mkuu Hemed Suleiman amewajumuisha wachezaji waandamizi na vijana chipukizi kutoka klabu mbalimbali za Ligi Kuu Tanzania Bara kama vile Simba, Yanga, Azam FC, Coastal Union, Singida Big Stars, na JKT Tanzania, pamoja na nyota kutoka timu ya vijana ya Ngorongoro Heroes.

Walinda Mlango Walioteuliwa

Wachezaji watatu wamechaguliwa kuongoza safu ya ulinzi langoni:

  • Aishi Manula (Simba SC)
  • Hussein Masalanga (Singida Big Stars)
  • Yakoub Suleiman (JKT Tanzania)

Mabeki Watakaoongoza Ngome

Safu ya ulinzi imejumuisha mabeki wenye uzoefu na chipukizi:

  • Shomari Kapombe (Simba SC)
  • Lusajo Mwaikenda (Azam FC)
  • Mohamed Hussein (Simba SC)
  • Paschal Msindo (Azam FC)
  • Wilson Nangu (JKT Tanzania)
  • Vedastus Masinde (U20 Ngorongoro Heroes/TMA)
  • Ahmed Pipino (U20 Ngorongoro Heroes/KMC)
  • Yusuph Kagoma (Simba SC)

Viungo Watakaoshika Usukani Kati ya Uwanja

Kocha Hemed amewaita viungo wenye uwezo mkubwa wa kuendesha mchezo:

  • Ibrahim Hamad (Young Africans)
  • Dickson Job (Young Africans)
  • Mudathir Yahya (Young Africans)
  • Feisal Salum (Azam FC)
  • Nassor Saadun (Azam FC)
  • Sabry Kondo (Coastal Union)
  • Sheikhan Khamis (U20 Ngorongoro Heroes/Young Africans)
  • Clement Mzize (Young Africans)
  • Mishano Michael (U20 Ngorongoro Heroes/Kengold FC)
  • Ibrahim Hamad (Tabora United)

Washambuliaji Watakaotegemewa Kufumania Nyavu

Katika safu ya ushambuliaji, majina haya yatakuwa na jukumu la kusaka mabao:

  • Abdulrazack Mohamed (Simba SC)
  • Kibu Denis (Simba SC)
  • Lameck Lawi (Coastal Union)
  • Jammy Simba (U20 Ngorongoro Heroes/KMC)
  • Iddy Selemani (Azam FC)
  • Abdul Suleiman (Azam FC)

Taifa Stars Kuwania Ubingwa wa CHAN Afrika Mashariki

Wachezaji hao watajiunga kambini nchini Misri kwa mazoezi ya mwisho kabla ya kuanza kwa mashindano ya CHAN 2024, ambayo yanatoa nafasi kwa wachezaji wa ligi za ndani kuonyesha vipaji vyao kimataifa. Ushiriki wa Tanzania ni nafasi muhimu ya kukuza vipaji na kuleta heshima kwa taifa.

🔔 Je? unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!

🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!