Michezo

Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa Leo 2025 Kufuzu Kombe la Dunia

Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa Septemba 2025 Kufuzu Kombe la Dunia

Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa Septemba 2025

Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Hemedi Moroco, ametangaza rasmi kikosi cha Taifa Stars kitakachoshiriki mechi mbili muhimu za kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Congo na Niger mwezi Septemba 2025.

Mabadiliko Ndogo Kwenye Kikosi

Hakuna mabadiliko makubwa kwenye kikosi hiki ikilinganishwa na kikosi kilichopita, jambo linaloonyesha imani kubwa ya makocha kwa wachezaji waliopo. Timu inatarajiwa kushirikiana kwa karibu kuhakikisha inapata angalau pointi 4 katika michezo hii miwili, jambo litakaloiweka katika nafasi nzuri ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia ya soka la Tanzania.

Wachezaji Walioitwa

  • Yakoub Suleiman (JKT Tanzania)
  • Hussein Masaranga (Singida BS)
  • Antony Remmy (Azam FC U20)
  • Shomari Kapombe (Simba SC)
  • Lusajo Mwaikenda (Azam FC)
  • Wilson Nangu (JKT Tanzania)
  • Mohamed Hussein (Young Africans)
  • Pascal Msindo (Azam FC)
  • Ibrahim Abdulla (Young Africans)
  • Dickson Job (Young Africans)
  • Yusuph Kagoma (Simba SC)
  • Novatus Dismas (Gรถztepe FC, Uturuki)
  • Yahya Zaid (Azam FC)
  • Edmund John (Young Africans)
  • Charles Mโ€™Mombwa (Floriana FC, Malta)
  • Mudathir Yahya (Young Africans)
  • Clement Mzize (Young Africans)
  • Mbwana Samatta (Le Havre AC, Ufaransa)
  • Abdul Hamis (Azam FC)
  • Feisal Salum (Azam FC)
  • Saimon Msuva (Al-Talaba SC, Iraq)
  • Iddy Selemani (Azam FC)
  • Selemani Mwalimu (Simba SC)

Kocha Mkuu: Hemed Suleiman

Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa Septemba 2025 Kufuzu Kombe la Dunia
Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa Septemba 2025 Kufuzu Kombe la Dunia

Ratiba ya Mechi za Taifa Stars โ€“ Septemba 2025

  • 02 Septemba 2025: Congo Brazzaville ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฌ vs Tanzania ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
  • 09 Septemba 2025: Tanzania ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ vs Niger ๐Ÿ‡ณ๐Ÿ‡ช

Mashabiki wa soka wanatarajiwa kufuatilia mechi hizi kwa shauku, wakitarajia kuona Taifa Stars ikicheza kwa nidhamu na kujitahidi kupata matokeo mazuri. Ushindi nyumbani dhidi ya Congo na sare angalau ugenini utakuwa hatua kubwa kuelekea kufuzu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza.