Michezo

Kikosi cha Taifa Stars vs Zambia Leo Oktoba 8 2025 – Kombe la Dunia 2026

Kikosi cha Taifa Stars vs Zambia Leo Oktoba 8 2025 – Kombe la Dunia 2026

Kikosi cha Taifa Stars vs Zambia Leo Oktoba 8 2025

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo Oktoba 8, 2025, inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, kuivaa Zambia katika mchezo muhimu wa kufuzu Kombe la Dunia 2026. Mchezo huo utaanza saa 4 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (22:00 EAT) na unatarajiwa kuvutia hisia kubwa kutokana na umuhimu wake katika mbio za kufuzu.

Maandalizi na Kauli ya Kocha Hemed “Morocco” Suleiman

Kocha mkuu Hemed “Morocco” Suleiman ametangaza kikosi kilichopangwa kwa umakini mkubwa, kikiwa na mchanganyiko wa wachezaji wenye uzoefu na nyota wapya. Akizungumza kabla ya mechi, Hemed alithibitisha changamoto ya majeruhi ndani ya kikosi, hasa kwa baadhi ya wachezaji muhimu.

“Tunakosa huduma za beki wetu Dickson Job kutokana na majeraha ya misuli ya paja, lakini tuna wachezaji wengine wenye uwezo wa kujaza nafasi hiyo na kuendeleza mpango wetu wa kimkakati,” alisema Kocha Hemed Morocco.

Kikosi cha Taifa Stars Dhidi ya Zambia Leo

Kikosi cha Taifa Stars kwa mchezo huu kina jumla ya wachezaji 26, wakiwemo makipa watatu, mabeki kumi, viungo saba na washambuliaji sita. Idadi kubwa ya mabeki inaonyesha dhamira ya benchi la ufundi kuimarisha ukuta wa timu hiyo dhidi ya wapinzani wao wenye nguvu, Zambia.

Makipa

  • Yakoub Suleiman
  • Hussein Masalanga
  • Zuberi Foba

Mabeki

  • Lusajo Mwaikenda
  • Bakari Mwamnyeto
  • Lameck Lawi
  • Miano Danilo
  • Haji Mnoga
  • Wilson Nangu
  • Pascal Msindo
  • Ibrahim Abdulla
  • Novatus Dismas

Viungo

  • Aziz Andabwile
  • Yahya Zayd
  • Yusuph Kagoma
  • Feisal Salum
  • Halid Habibu
  • Habibu Idd
  • Morice Abraham

Washambuliaji

  • Charles Mmombwa
  • Suleiman Mwalimu
  • Edwin Balua
  • Offen Chikola
  • Tarryn Allarakhia

Wachezaji Walio Rejea na Waliosalia Nje

Baadhi ya wachezaji waliokuwa hawajaitwa kwa muda mrefu kama Haji Mnoga, Miano Danilo, Offen Chikola, Habibu Khalid, Aziz Andabwile, Tarryn Allarakhia na Edwin Balua wamerejea, hatua inayotarajiwa kuongeza ushindani na nguvu mpya ndani ya kikosi.
Hata hivyo, majina makubwa kama Aishi Manula, Mbwana Samatta, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein na Simon Msuva hayajumuishwi katika kikosi hiki, jambo lililosababisha mshangao kwa baadhi ya mashabiki. Vilevile, Abdulrazack Hamza wa Simba na Ahmed Pipino wa KMC hawajaitwa kutokana na majeraha na sababu za kiufundi.

Umuhimu wa Mchezo wa Leo

Mchezo huu dhidi ya Zambia ni wa mwisho kwa Taifa Stars katika kundi E la kufuzu Kombe la Dunia 2026. Tanzania inahitaji ushindi ili kufikisha pointi 13, jambo litakaloiweka katika nafasi ya pili nyuma ya vinara Morocco. Kumaliza katika nafasi hiyo kutaiweka Taifa Stars katika nafasi nzuri ya kuwania moja ya nafasi nne za mchujo (playoffs) kwa timu za Afrika zitakazopigania tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazofanyika Canada, Mexico na Marekani.