Michezo

Kikosi cha Yanga Vs Simba Leo 16/09/2025 Ngao ya Jamii

Kikosi cha Yanga Vs Simba Leo 16/09/2025
Kikosi cha Yanga Vs Simba Leo 16/09/2025

Yanga Vs Simba Leo: Fainali ya Ngao ya Jamii 2025

Leo Septemba 16, 2025, fainali ya Ngao ya Jamii inachezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam ikiwakutanisha mahasimu wa jadi Yanga SC na Simba SC. Huu ni mchezo wa ufunguzi wa msimu wa 2025/2026 unaotarajiwa kuvuta mashabiki wengi, ukipambwa na ushindani wa kijani na nyekundu.

Kikosi cha Yanga Vs Simba Leo 16/09/2025

  • 39 DIARRA
  • 23 BOKA
  • 33 MWENDA
  • 5 JOB
  • 4 BACCA
  • 38 ABUYA
  • 7 MAXI
  • 2 ANDABWILE
  • 29 DUBE
  • 27 MUDATHIR
  • 10 PACOME

SUBSTITUTES:

Mshery, Mwamnyeto, Ninju, Hussein, Abdulnassir, Conte, Kouma, Doumbia, Ecua, Mzize

Kikosi cha Yanga Vs Simba Leo 16/09/2025
Kikosi cha Yanga Vs Simba Leo 16/09/2025

Mfumo Mpya wa Ngao ya Jamii

Tofauti na msimu uliopita ulioshirikisha timu nne, mwaka huu fainali hii imechezwa kwa mtindo wa mchezo mmoja pekee. TFF ilipunguza idadi ya mechi kutokana na ratiba ya kitaifa na kimataifa, ikiwemo CHAN 2025 na mchujo wa Kombe la Dunia kwa Taifa Stars.

Kikosi cha Simba SC kitapangwa na kutangazwa na benchi la ufundi saa moja kabla ya mpira kuanza.

Historia ya Ngao ya Jamii

Ngao ya Jamii ilianzishwa mwaka 2001 kwa pambano la Yanga dhidi ya Simba ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa 2-1. Simba imefanikiwa kutwaa Ngao mara 10, huku Yanga ikiibeba mara 8. Katika fainali tisa zilizowakutanisha, Simba imeshinda tano na Yanga mara nne.

Nani Ataibuka Kidedea Leo?

Fainali ya leo ni zaidi ya pambano la ufunguzi wa msimu. Ni vita ya rekodi, heshima na mwanzo mpya wa mashindano. Mashabiki wanatarajia burudani ya aina yake huku historia ikiandikwa tena Uwanja wa Benjamin Mkapa.