Orodha ya Kozi za VETA na Gharama Zake 2025
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inaendelea kuimarisha maendeleo ya ujuzi nchini kwa kutoa kozi mbalimbali zenye mwelekeo wa vitendo. Kozi hizi zimegawanyika katika makundi mawili: muda mrefu na muda mfupi, na zinalenga kuongeza fursa za ajira kwa vijana wa Kitanzania.
Kozi za Muda Mrefu VETA 2025
Kozi hizi huchukua kati ya miezi 3 hadi 6, kulingana na fani unayochagua. Ada ya mwanafunzi wa kutwa ni TSh 60,000 na kwa mwanafunzi wa bweni ni TSh 120,000. Gharama nyingine zinazohusiana na vifaa na huduma hulipwa kati ya TSh 200,000 hadi 250,000 kutegemeana na chuo na kozi husika.
Mifano ya Kozi za Veta za Muda Mrefu
Ufundi wa Magari
- Muda: Miezi 6
- Ada: TSh 355,000
- Chuo: VETA Chato
Umeme wa Majumbani
- Muda: Miezi 6
- Ada: TSh 355,000
- Chuo: VETA Chato
Ushonaji wa Nguo
- Muda: Miezi 5
- Ada: TSh 355,000
- Chuo: VETA Chato
Matumizi ya Kompyuta
- Muda: Miezi 3
- Ada: TSh 165,000
- Chuo: VETA Chato
Ufundi Bomba
- Muda: Miezi 6
- Ada: TSh 355,000
- Chuo: VETA Chato
Kozi za VETA za Muda Mfupi 2025
Hizi ni kozi zinazochukua wiki 1 hadi miezi 3, zikitolewa kwa ajili ya kuwapa wahusika ujuzi wa haraka katika fani maalum. Ada za kozi hizi zinatofautiana kati ya TSh 50,000 hadi 320,000 kutegemeana na kozi na chuo.
Mifano ya Kozi za Muda Mfupi
Udereva wa Awali
- Muda: Wiki 5
- Ada: TSh 200,000
- Chuo: VETA Mbeya
Udereva wa Magari ya Abiria (PSV)
- Muda: Wiki 2
- Ada: TSh 200,000
- Chuo: VETA Mbeya
Udereva wa Pikipiki na Bajaji
- Muda: Wiki 2
- Ada: TSh 70,000
- Chuo: VETA Mbeya
Uhazili (Kompyuta na Sekretarieti)
- Muda: Miezi 3
- Ada: TSh 200,000
- Chuo: VETA Mbeya
Tecknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT)
- Muda: Miezi 5
- Ada: TSh 600,000
- Chuo: VETA Mbeya

Utaratibu wa Kujiunga na Kozi za VETA
Kwa yeyote anayetaka kujiunga na mafunzo ya VETA, ni muhimu kufuata taratibu rasmi zifuatazo:
Hatua za Kujiunga
1. Kupata Fomu ya Maombi
Fomu zinapatikana kwenye vyuo vya VETA au kupitia tovuti yao rasmi.
2. Kujaza Fomu kwa Usahihi
Hakikisha taarifa zako zote zimejazwa kikamilifu na kwa usahihi.
3. Kuambatisha Nyaraka
Ambatanisha nakala ya cheti cha elimu, cheti cha kuzaliwa, na picha za pasipoti.
4. Kuwasilisha Maombi
Wasilisha fomu kamili pamoja na nyaraka zote kwenye chuo husika cha VETA unachotaka kujiunga nacho.
5. Kufanya Mtihani wa Kujiunga
Baada ya kuwasilisha maombi, utahitajika kufanya mtihani wa kujiunga kama sehemu ya mchakato wa kuchagua wanafunzi.
VETA inaendelea kuwa chaguo bora kwa watanzania wanaotaka kupata elimu ya ufundi yenye tija na inayolingana na soko la ajira.
🔔 Je? unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!