Majina ya Waliochaguliwa Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS) 2025/2026
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimetoa rasmi orodha ya majina ya waombaji waliochaguliwa kujiunga na masomo kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Hii ni taasisi maarufu ya elimu ya juu nchini Tanzania inayotoa kozi za afya na sayansi shirikishi kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza na Shahada za Juu.
Waombaji waliokidhi vigezo vya udahili wametangazwa kupitia orodha rasmi inayopatikana kwenye tovuti ya chuo.
Selected Candidates for Bachelor Programs Academic Year 2025/ 2026
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa MUHAS
Kupitia Tovuti Rasmi ya MUHAS
- Tembelea tovuti: www.muhas.ac.tz
- Nenda sehemu ya Announcements/News
- Tafuta tangazo lenye kichwa “MUHAS Selected Applicants 2025/2026”
- Pakua faili la PDF lenye orodha ya majina
- Fungua PDF na tumia kipengele cha kutafuta (Ctrl + F) ili kuangalia jina lako
👉 Bonyeza hapa kuangalia majina ya waliochaguliwa MUHAS 2025/26
Kupitia Mfumo wa Maombi ya Mtandaoni
- Tembelea: saris2.muhas.ac.tz
- Ingia kwa jina la mtumiaji na nenosiri ulilotumia kuomba chuo
- Angalia sehemu ya Application Status / Hali ya Maombi
- Pakua Barua ya Udahili na Joining Instructions ikiwa umechaguliwa
Hatua Baada ya Kuchaguliwa MUHAS
- Thibitisha Udahili: Fanya uthibitisho kupitia mfumo wa TCU au mfumo wa MUHAS ndani ya muda uliopangwa
- Pakua Barua ya Udahili: Pata barua rasmi ya udahili pamoja na maelekezo ya kujiunga chuoni
- Andaa Nyaraka Muhimu: Vyeti vya elimu, cheti cha kuzaliwa, picha za pasipoti na kitambulisho cha taifa
- Fanya Malipo: Lipa ada na gharama nyingine kwa njia zilizotolewa na chuo
Jinsi ya Kuthibitisha Udahili MUHAS
- Pokea Special Code kutoka TCU kupitia SMS
- Ingia saris2.muhas.ac.tz kwa akaunti yako
- Ingiza “Special Code” kisha bonyeza Confirm
- Pokea ujumbe wa mafanikio kuthibitisha kuwa udahili wako umekamilika
Kwa orodha kamili ya waliochaguliwa MUHAS 2025/26, pakua faili la PDF kupitia tovuti rasmi ya MUHAS au angalia kupitia mfumo wa maombi ya mtandaoni.