Majina ya Waliochaguliwa UDOM 2025/2026
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimetangaza rasmi orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Orodha hii inajumuisha wanafunzi waliofaulu na kukidhi vigezo vya udahili kwa programu za shahada na stashahada.
Link za Kupakua PDF za Waliochaguliwa
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa UDOM
1. Kupitia Tovuti Rasmi ya UDOM
- Tembelea tovuti ya UDOM
- Nenda kwenye sehemu ya Matangazo au Habari
- Tafuta tangazo lenye kichwa Majina ya Waliochaguliwa 2025/26
- Pakua faili ya PDF na utafute jina lako
2. Kupitia Mfumo wa Maombi UDOM (OAS)
- Fungua UDOM OAS
- Ingia kwa kutumia username na password ulizotumia kuomba
- Angalia sehemu ya Admission Status
- Pakua Barua ya Udahili na Joining Instructions
Hatua Baada ya Kuchaguliwa
- Kuthibitisha Udahili: Luthibitisha nafasi yako ndani ya muda uliopangwa ili usipoteze nafasi
- Kupakua Barua ya Udahili: Pata barua rasmi yenye maelekezo ya kujiunga
- Maandalizi: Hakikisha unakamilisha nyaraka muhimu (vyeti, cheti cha kuzaliwa, picha za pasipoti) na kufanya malipo ya ada
Jinsi ya Kuthibitisha Udahili UDOM
- Pokea SPECIAL CODE kupitia SMS kutoka UDOM
- Ingia UDOM OAS kwa username na password yako
- Ingiza SPECIAL CODE na thibitisha
- Ukiona ujumbe wa mafanikio, udahili wako umekamilika
Kwa kufuata hatua hizi, utaweza kuthibitisha nafasi yako na kuanza safari ya elimu ya juu katika UDOM msimu wa masomo 2025/2026. Tunakutakia mafanikio mema katika masomo yako!