Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Vyuo Vikuu 2025/2026
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kukamilika kwa Awamu ya Kwanza ya udahili wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2025/2026 katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini.
Takwimu za Udahili 2025/2026
- Idadi ya waombaji: 146,879 walituma maombi kujiunga na vyuo 88 vilivyoidhinishwa.
- Idadi ya programu: 894 zimeruhusiwa kudahili wanafunzi, ongezeko la programu 38 kutoka 856 mwaka 2024/2025.
- Nafasi zilizotolewa: 205,652 ikilinganishwa na 198,986 mwaka uliopita, ongezeko la nafasi 6,666 sawa na asilimia 3.3.
- Waliopata nafasi: 116,596 sawa na asilimia 79.4 ya waombaji wote wamepata udahili katika vyuo walivyoomba.
Orodha ya Majina ya Waliochaguliwa Vyuo Vikuu
Majina ya wanafunzi waliopata udahili katika awamu hii yametangazwa na vyuo husika. Idadi ya waliochaguliwa inatarajiwa kuongezeka baada ya Awamu ya Pili ya udahili kukamilika.
📄 Pakua Orodha ya Waliochaguliwa Kujiunga na Chuo Zaidi ya Kimoja au Programu Zaidi ya Moja 2025/2026