Elimu

Majina ya Waliochaguliwa Zaidi ya Chuo Kimoja au Programu 2025/2026 TCU

Majina ya Waliochaguliwa Zaidi ya Chuo Kimoja au Programu 2025/2026

Majina ya Waliochaguliwa Zaidi ya Chuo Kimoja au Programu 2025/2026

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kuwa Awamu ya Kwanza ya udahili wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2025/2026 imekamilika rasmi. Hatua hii inahusisha vyuo vikuu na taasisi 88 za elimu ya juu vilivyoidhinishwa kudahili wanafunzi nchini.

Takwimu za Udahili Awamu ya Kwanza

  • Jumla ya waombaji 146,879 walituma maombi ya kujiunga.
  • Programu zilizoruhusiwa: 894 (ongezeko kutoka 856 mwaka 2024/2025).
  • Nafasi za udahili zilizotolewa: 205,652 ikilinganishwa na 198,986 mwaka uliopita (ongezeko la nafasi 6,666 sawa na 3.3%).
  • Jumla ya 116,596 waombaji sawa na 79.4% ya waliotuma maombi walichaguliwa katika awamu hii ya kwanza.

Idadi hii inatarajiwa kuongezeka zaidi katika Awamu ya Pili ya udahili.

Waliodahiliwa Zaidi ya Chuo Kimoja

Waombaji waliochaguliwa zaidi ya chuo au programu moja wanapaswa kuthibitisha chuo kimojawapo kuanzia 03 hadi 21 Septemba 2025.

Hatua za Kuthibitisha Udahili

  1. Tumia namba ya siri iliyotumwa kupitia SMS au barua pepe wakati wa maombi.
  2. Ikiwa hujapokea ujumbe, ingia kwenye mfumo wa udahili wa chuo ulichodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mpya wa uthibitisho.
  3. Hakikisha unathibitisha kupitia akaunti ya udahili uliyotumia wakati wa kutuma maombi.

Orodha ya Majina

Kwa orodha kamili ya majina ya waombaji waliodahiliwa zaidi ya chuo kimoja au programu zaidi ya moja kwa mwaka wa masomo 2025/2026, bofya link hapa chini: