Kuitwa Kazini

Majina ya Walioitwa Kazini Serikalini 19 Julai 2025

Majina ya Walioitwa Kazini Serikalini 19 Julai 2025

Orodha ya Majina ya Walioitwa Kazini Serikalini 19 Julai 2025 imetangazwa. Soma jinsi ya kupakua barua za kazi na taratibu za kuripoti mahali pa kazi.

Majina ya Walioitwa Kazini Serikalini 19 Julai 2025

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ametangaza majina ya waombaji kazi waliopata nafasi baada ya usaili uliofanyika kati ya tarehe 5 Februari 2025 na 26 Juni 2025. Orodha hii pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (database) ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Jinsi ya Kupata Barua za Kupangiwa Kazi

Waombaji wote waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi wanapaswa kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal sehemu ya My Applications ili kupakua na kuchapisha barua zao za kupangiwa vituo vya kazi. Barua hizi ni muhimu kwa ajili ya kuripoti kwenye vituo vya kazi vilivyowekwa.

Taratibu za Kuripoti Mahali pa Kazi

Waombaji walioitwa kazini wanatakiwa kuripoti kwa mwajiri ndani ya muda uliotangazwa kwenye barua zao za kupangiwa kazi. Wanapaswa kuleta vyeti halisi vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe kabla ya kupewa barua rasmi ya ajira.

Kwa Waombaji Wasiojumuishwa Orodhani

Waombaji ambao majina yao hayapo katika orodha hii wanatakiwa kujiandaa kwa nafasi mpya zitakazotangazwa baadaye kwani hawakupata nafasi au hawakufaulu usaili huu. Wanaweza kuomba tena wakati nafasi mpya zitakapojitokeza.

Pakua Orodha Kamili ya Majina

Kwa orodha kamili ya walioshinda nafasi za kazi serikalini, bonyeza hapa kupakua PDF:
Majina ya Walioitwa Kazini 19 Julai 2025

🔔 Tafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya za ajira kila siku!