Majina ya Walioitwa Kazini Utumishi 02 Septemba 2025
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ametangaza majina ya waombaji kazi waliofaulu usaili uliofanyika kati ya 02 Novemba 2024 hadi 12 Juni 2025. Waombaji waliopata nafasi wamepangiwa vituo vya kazi katika taasisi mbalimbali za umma kuanzia tarehe 02 Septemba 2025.
Waliofanikiwa na Kanzidata
Mbali na waliopita kwenye usaili, tangazo hili pia linajumuisha baadhi ya waombaji waliokuwemo kwenye kanzidata (Database) ya Sekretarieti kwa kada mbalimbali, ambao sasa wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kufunguka.
Angalia Orodha Kamili ya Majina
Kwa majina ya walioitwa kazini pamoja na vituo walivyopangiwa, bofya kiungo kilichoambatanishwa hapa chini ili kuona tangazo rasmi:
DOWNLOAD Majina ya Walioitwa Kazini Utumishi 02 Septemba 2025 (PDF)