Matokeo ya Simba vs Kagera Sugar Leo 22 Juni 2025
Matokeo Simba vs Kagera Sugar Leo: Simba SC inashuka dimbani leo Jumapili tarehe 22 Juni 2025 saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, kukabiliana na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League). Hii ni mechi muhimu mno kwa Simba ambayo inahitaji ushindi ili kubaki kwenye mbio za ubingwa.
Simba Wapigania Ushindi Muhimu wa Mwisho wa Msimu
Wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, Simba SC wanaingia uwanjani kwa lengo moja tu—kuondoka na alama tatu. Ushindi huu utawaweka karibu na viongozi wa ligi katika siku ya mwisho ya msimu, hivyo kuweka presha ya ushindi kwa wapinzani wao.
Kagera Sugar Wacheza Bila Presha
Kagera Sugar tayari wamepoteza nafasi ya kubaki Ligi Kuu, wakishika nafasi ya 15. Timu hiyo imethibitishwa kushuka daraja na msimu ujao itashiriki Ligi Daraja la Kwanza. Kwa hali hiyo, wanaingia uwanjani bila presha yoyote, jambo ambalo linaweza kuwafanya kuwa wapinzani hatari kutokana na uhuru wa kucheza bila presha.

Hali ya Mechi Mubashara (LIVE)
SIMBA 1-0 KAGERA SUGAR
Mechi imeanza saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Simba SC wanapaswa kuwa makini dhidi ya Kagera Sugar, kwani wapinzani wao hawana la kupoteza. Hali hii mara nyingi huwaletea changamoto timu zinazopigania kitu kikubwa, hasa kama ubingwa, kwa kuwa timu zilizo huru hucheza kwa ubunifu na ari ya kufunga pazia kwa heshima.
🔔 Je? unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!