Michezo

Matokeo ya Yanga vs Singida Black Stars Leo 29/06/2025

Matokeo ya Yanga vs Singida Black Stars Leo

Matokeo ya Yanga vs Singida Black Stars Leo 29/06/2025 | Matokeo ya Yanga leo Dhidi ya Singida Black Stars Fainali. Timu ya Wananchi, Yanga SC, inatarajiwa kushuka tena dimbani leo Jumapili, tarehe 29 Juni 2025, kuwania taji la Kombe la Shirikisho la CRDB Federation Cup, ikiwa ni baada ya kukamilisha rasmi safari ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya NBC mnamo tarehe 25 Juni kwa kuichapa Simba SC mabao 2-0. Fainali ya leo dhidi ya Singida Black Stars imepangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, kuanzia saa 2:15 usiku (20:15), ikiwa ndiyo mchezo wa mwisho wa msimu wa 2024/2025 kwa klabu zote mbili.

Matokeo ya Yanga vs Singida Black Stars Leo 29/06/2025 – Nini Kinasubiriwa?

Mchezo huu wa fainali unatarajiwa kuwa wa ushindani mkali kati ya mabingwa watetezi Yanga na Singida BS wanaosaka taji lao la kwanza la kitaifa. Wakati mashabiki wakisubiri matokeo ya Yanga vs Singida Black Stars leo 29/06/2025, macho yote yataelekezwa Zanzibar, ambako historia mpya inaweza kuandikwa baada ya dakika 90 au zaidi ikiwa kutahitajika muda wa nyongeza au mikwaju ya penalti.

Matokeo ya Yanga vs Singida Black Stars Leo
Matokeo ya Yanga vs Singida Black Stars Leo 29/06/2025

Matarajio Ya Mchezo – Saa 2:15 Usiku Zanzibar

Fainali hii inatarajiwa kuchezwa kwa kasi na nidhamu ya hali ya juu, ikizingatiwa uzoefu wa makocha wote wawili. Miloud Hamdi, ambaye aliwahi kuifundisha Singida mwishoni mwa mwaka 2024 kabla ya kujiunga na Yanga, atakuwa na nia ya kutwaa taji la pili msimu huu akiwa na klabu hiyo. Kwa upande mwingine, David Ouma wa Singida anataka kufanikisha malengo yake ya kuifikisha timu hiyo kileleni kwa mara ya kwanza.

Kwa mujibu wa mwenendo wa mechi zao zilizopita, mabao mengi yanatarajiwa kufungwa kipindi cha pili. Yanga imekuwa na uwiano sawa wa mabao kipindi cha kwanza na pili, ilhali Singida imekuwa tishio zaidi kipindi cha pili.

🔔 Je? unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!

🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!