Nafasi 127 za Ufadhili wa Masomo Saudi Arabia 2025/2026
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imepokea kwa furaha taarifa kutoka Ufalme wa Saudi Arabia kuhusu kutolewa kwa nafasi 127 za ufadhili wa masomo ya shahada ya uzamili kwa mwaka wa masomo 2025/2026, kwa ajili ya wanafunzi wa Kitanzania.
Masomo Kufanyika Katika Vyuo Mbalimbali Saudi Arabia
Ufadhili huu utatekelezwa kupitia vyuo vikuu mbalimbali vilivyopo nchini Saudi Arabia, ambapo kila chuo kitakuwa na taratibu zake za udahili kulingana na aina ya programu.
Waombaji wanaotaka kusomea fani za kisasa na zenye ushindani mkubwa kimataifa wanahimizwa kuwasilisha maombi yao mapema, hasa kwa wale walio na nia ya kusomea:
- Sayansi ya Data
- Akili Bandia (Artificial Intelligence)
- Sayansi Shirikishi (Integrated Sciences)
Taarifa Rasmi ya Tangazo
Kwa maelezo kamili kuhusu vigezo vya kuomba, vyuo vinavyotoa ufadhili, na taratibu zote za maombi, download tangazo rasmi la wizara kupitia kiungo hapa chini:
📄 Download Tangazo la Saudi Arabia 2025/2026 (PDF)
TCheki tangazo hilo kwa:
- Orodha ya vyuo vinavyotoa ufadhili
- Tarehe muhimu za kuwasilisha maombi
- Hati na sifa zinazotakiwa
- Jinsi ya kuwasiliana kwa maswali au msaada
Kwa habari zaidi kuhusu fursa za masomo nje ya nchi, endelea kufuatilia taarifa mpya kupitia tovuti ya Wizara ya Elimu au mitandao ya serikali.
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!
🔔 Kwa habari mpya Kila siku. Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya habari kila siku!