Fursa za Kazi Mpya Muheza 2025: Nafasi 15 Zatangazwa Rasmi
Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imetangaza nafasi 15 za kazi baada ya kupata kibali rasmi cha ajira kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Tangazo hili linawahusu Watanzania wote wenye sifa stahiki waliopo ndani na nje ya nchi.
Nafasi zinazopatikana ni pamoja na:
- Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II (Nafasi 5): Anatakiwa awe na elimu ya kidato cha Nne au Sita, cheti cha Uhazili (NTA Level 6), uwezo wa kuchapa maneno 100 kwa dakika kwa Kiswahili na Kiingereza pamoja na ujuzi wa kompyuta.
- Dereva Daraja la II (Nafasi 6): Mwombaji awe na elimu ya kidato cha Nne, leseni ya Daraja E au C, uzoefu wa mwaka mmoja bila ajali na cheti cha mafunzo ya udereva kutoka chuo kinachotambulika kama VETA.
- Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II (Nafasi 4): Awe na Stashahada ya utunzaji kumbukumbu (NTA Level 6), elimu ya kidato cha Nne au Sita na ujuzi wa kompyuta.
Waombaji wote wanapaswa kuwa Watanzania wenye umri wa miaka 18 hadi 45 na kuambatanisha vyeti vya kuzaliwa, taaluma, picha mbili za passport, CV iliyo kamili pamoja na barua ya maombi iliyoandikwa rasmi ikielekezwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira Portal.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA TANGAZO
Mwisho wa kutuma maombi: 01 Julai 2025.
Masharti ya Jumla kwa Waombaji
- Raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 hadi 45
- Kuambatanisha vyeti vya kuzaliwa, taaluma, na CV iliyo na maelezo ya kina
- Picha mbili za passport za karibuni
- Vyeti vya elimu ya nje ya nchi vihalalishwe na NECTA, TCU au NACTE
- Wastaafu wa umma hawaruhusiwi bila kibali maalum
- Vyeti vya udereva vya madaraja yanayohusika viambatishwe
- Barua ya maombi ya kazi iwekwe kwenye mfumo wa Ajira Portal
Tarehe ya Mwisho ya Kutuma Maombi
Maombi yote yawasilishwe kabla ya tarehe 01 Julai, 2025 kupitia:
👉 https://portal.ajira.go.tz
Anuani ya Barua:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Muheza,
S.L.P. 20,
Muheza.
Imetolewa na:
Dr. Jumaa M. Mhina
Mkurugenzi Mtendaji – Halmashauri ya Wilaya Muheza
🔔 Unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!