Ajira

NAFASI 8 Za Kazi Ikungi District Council

NAFASI 8 Za Kazi Ikungi District Council

Nafasi 8 Mpya za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi – Maombi Kabla ya 1 Julai 2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ametangaza ajira mpya kufuatia kibali kilichotolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia Kumb. Na. FA.97/228/01/A/25 ya tarehe 29 Aprili 2025.

Fursa hizi zinapatikana kwa Watanzania wote wenye sifa zinazostahiki, na maombi yote yanapaswa kuwasilishwa kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa Ajira Portal.

Nafasi Zilizotangazwa na Idadi ya Nafasi

1. Dereva Daraja la Pili – Nafasi 4
Waombaji wanapaswa kuwa na uzoefu na sifa stahiki kwa kazi za udereva kama zilivyoainishwa kwenye tangazo rasmi.

2. Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la Pili – Nafasi 2
Kazi hii inahitaji uwezo wa kushughulikia nyaraka na kumbukumbu ofisini kwa umakini na weledi.

3. Mhudumu wa Jikoni Daraja la Pili – Nafasi 2
Nafasi hii ni kwa wale wenye uzoefu wa kazi za jikoni katika taasisi au mazingira ya kiofisi.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Maombi yote yanapaswa kutumwa kupitia mfumo rasmi wa Ajira Portal. Waombaji wote wanatakiwa:

  • Kujiandikisha au kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal
  • Kujaza fomu ya maombi kwa usahihi
  • Kuweka viambatisho vyote muhimu kama ilivyoelekezwa kwenye mfumo

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 1 Julai 2025

Waombaji wanakumbushwa kuhakikisha wanafuata maelekezo yote yaliyopo kwenye tangazo. Ni muhimu kuwasilisha maombi mapema kabla ya muda kuisha.

🔔 Unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!

🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!