NMB Bank PLC Yatangaza Nafasi 8 za Kazi Mpya – Tuma Maombi Kabla ya Juni 25, 2025
Nafasi Mpya za Kazi NMB Bank PLC – Juni 2025
NMB Bank PLC, mojawapo ya taasisi kubwa za kifedha nchini Tanzania, imefungua milango kwa waombaji wa ajira 8 katika maeneo mbalimbali ya kitaalamu. Benki hii ya biashara imeidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania na inatoa huduma kwa watu binafsi, biashara ndogo na za kati, kampuni pamoja na wateja wakubwa wa biashara.
Kwa mujibu wa takwimu za Septemba 2023, NMB ilikuwa benki ya pili kwa ukubwa nchini kwa mtaji, ikifuatia CRDB Bank PLC.
Benki hiyo sasa inawakaribisha Watanzania wenye uwezo, uzoefu na sifa zinazohitajika kutuma maombi ya nafasi mpya zilizotangazwa. Nafasi hizi ni kwa kandarasi ya muda maalum na baadhi ni za kudumu, kulingana na majukumu husika.
Nafasi za Kazi Zinazopatikana NMB
- Audit Associate – ICT and Data Analytics (Mkataba wa Miaka 2) – Nafasi 1
- Manager – Credit Operations (Wholesale, Syndication & SME’s) – Nafasi 1
- Manager – Head Office Audits – Nafasi 1
- Requests Management Analyst – Nafasi 1
- Senior Manager – ICT Audits & Data Analytics – Nafasi 1
- Specialist – Change & Configurations – Nafasi 1
- Specialist – Product Life Cycle Configuration – Nafasi 1
- Zonal Relationship Manager – Nafasi 1
Tarehe ya Mwisho ya Kutuma Maombi
Mwisho wa kutuma maombi ni Juni 25, 2025. Waombaji wanashauriwa kuwasilisha maombi yao mapema ili kuepuka usumbufu wa dakika za mwisho.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Kama una sifa zinazohitajika na nia ya kujiunga na taasisi kubwa ya kifedha nchini, unaweza kutuma maombi kupitia link rasmi ya NMB:
🔔 Tafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!